Tenzi za Rohoni 73 – Yesu Zamani Bethrehemu

Tenzi za Rohoni 73 – Yesu Zamani Bethrehemu

Tenzi Na. 73

Soma maneno kamili ya Tenzi za Rohoni namba 73, “Yesu Zamani Bethrehemu”, kwa ajili ya ibada, kuimba na kujifunza.


Maneno ya Wimbo

Yesu zama Bethrehemu,
Aliyezaliwa kwa aibu,
Ndiye mwakozi wa ulimwengu,
Akaja kwa mimi.
Akaja kwa mimi; akaja kwa mimi;
Ndiye mwaokozi wa ulimwengu,
Akaja kwa mimi.
Yesu akafa msalabani,
Kuniponya akalipa deni,
Ni la ajabu ya jinsi gani
Kunifia mimi!
Kunifia mimi! Kunifia mimi!
Ni la ajabu ya jinsi gani
Kunifia mimi.
Ni yeye huyo tangu asili;
Na nilipotanga-tanga mbali
Alikuja kwa upole, kweli
Kuniita mimi.
Kuniita mimi; Kuniita mimi;
Alikuja kwa upole, kweli
Kuniita mimi
Yesu kristo atarudi tena,
Hilo lanifurahisha sana.
Yeye Bwana akionekana
Kunijia mimi.
Kunijia mimi, kunijia mimi,
Yeye Bwana akionekana
Kunijia mimi


Tazama Tenzi za Rohoni 1–164


Omba App ya Tenzi za Rohoni kwa Android

banner
Scroll to Top