Tenzi za Rohoni 69 – Twendeni Askari

Tenzi za Rohoni 69 – Twendeni Askari

Tenzi Na. 69

Soma maneno kamili ya Tenzi za Rohoni namba 69, “Twendeni Askari”, kwa ajili ya ibada, kuimba na kujifunza.


Maneno ya Wimbo

Twendeni askari, watu wa Mungu;
Yesu yuko mbele, tumwandame juu.
Ametangulia Bwana vitani,
Twende mbele kwani ndiye amini.
Twende askari watu wa Mungu;
Yesu yuko Mbele, tumwandame juu.
Jeshi la Shetani, likisikia
Jina la Mwokozi, litakimbia,
Kelele za shangwe zivume nchi;
Ndugu inueni zenu sauti.
Kweli kundi dogo, watu wa Mungu
Sisi na mababa tu moja fungu.
Hatutengwi nao, moja imani,
Tumaini moja, na moja dini.
Haya mbele watu nasi njiani,
Inueni myoyo, nanyi sifuni;
Heshima na sifa ni ya Mfalme,
Juu hata chini, sana zivume.


Tazama Tenzi za Rohoni 1–164


Omba App ya Tenzi za Rohoni kwa Android

banner
Scroll to Top