Tenzi za Rohoni 65 – Safari
Tenzi za Rohoni 65 – Safari Tenzi Na. 65 Soma maneno kamili ya Tenzi za Rohoni namba 65, “Safari”, kwa ajili ya ibada, kuimba na kujifunza. Maneno ya Wimbo Katika safari yetu Kwenda Mbinguni Tusiishe siku zetu Usingizini. Ng’oani! Tujifungeni, Twende zetu juu! Kristo ndiye kiongozi; Tusihofu tu. Atwekwe badala yetu, Mwenyewe Bwana; Yesu kiongozi wetu Atapokea. Kisimani, maji tele, Maji mazima! Maji hayo, Ya milele Yana neema. Njiani miiba mingi, Yatuumiza; Hofu na hatari nyingi, Sana zakaza. Kweli, njia ya Mbinguni Ni ya mashaka; Tuwe na Yesu njiani, Mara hufika. ← Tenzi 64 | Tenzi Zote | Tenzi 66 → Tazama Tenzi za Rohoni 1–164 Omba App ya Tenzi za Rohoni kwa Android