Skip to main content

Author name: contact@devinevisiontech.com

Tenzi za Rohoni

Tenzi za Rohoni 55 – Nipe Moyo Wenye Sifa

Tenzi za Rohoni 55 – Nipe Moyo Wenye Sifa Tenzi Na. 55 Soma maneno kamili ya Tenzi za Rohoni namba 55, “Nipe Moyo Wenye Sifa”, kwa ajili ya ibada, kuimba na kujifunza. Maneno ya Wimbo Nipe moyo wenye sifa Sio wa utumwa; Moyo ulionyunyizwa Damu ya thamani. Moyo msikizi, moyo Wa kunyenyekea, Moyo utawaliwao Na Mwokozi pia. Mwenye kutubu, mnyonge, Sadiki, amini; Kamwe, kamwe asitengwe Akaaye ndani. Mpya, mwema na mawazo Mwingi wa mapenzi Nawe uwe kielelezo Moyo wa Mwokozi. Ni uule moyo wako; Moyo wa huruma Yesu, natamani kwako Kukujua vyema. Na ya midomo matunda Yako, nipe nami; Amani isiyokoma Iwe yangu mimi. Nitie yako tabia, Inishukie juu; Jina lako nipe pia, Ndilo la upendo. Ni wa baba utukufu; Mwana atukuke; Na roho Mtakatifu U utatu pweke. ← Tenzi 54 | Tenzi Zote | Tenzi 56 → Tazama Tenzi za Rohoni 1–164 Omba App ya Tenzi za Rohoni kwa Android

Tenzi za Rohoni

Tenzi za Rohoni 54 – Yesu Nataka Kutakaswa Sana

Tenzi za Rohoni 54 – Yesu Nataka Kutakaswa Sana Tenzi Na. 54 Soma maneno kamili ya Tenzi za Rohoni namba 54, “Yesu Nataka Kutakaswa Sana”, kwa ajili ya ibada, kuimba na kujifunza. Maneno ya Wimbo Yesu nataka kutakaswa sana, Nataka moyo uwe enzi yako. Ukiangushe kilichoinuka Unioshe sasa niwe mweupe. Mweupe tu, ndiyo mweupe, Ukiniosha nitakuwa safi. Bwaba Yesu, unitazame sasa, Unifanye niwe dhabihu hai; Najitoa kwako, na moyo wote; Unioshe sasa niwe mweupe. Bwana kwa hiyo nakuomba sana, Nakungojea miguuni pako, Naomba unioshe damuni tu, Unioshe sasa niwe mweupe. Bwana nidumu kukungojea, Niumbie moyo safi, Ee Mungu, Wanaokujia hutupi kamwe, Unioshe sasa niwe mweupe. ← Tenzi 53 | Tenzi Zote | Tenzi 55 → Tazama Tenzi za Rohoni 1–164 Omba App ya Tenzi za Rohoni kwa Android

Tenzi za Rohoni

Tenzi za Rohoni 53 – Wewe Umechoka Sana?

Tenzi za Rohoni 53 – Wewe Umechoka Sana? Tenzi Na. 53 Soma maneno kamili ya Tenzi za Rohoni namba 53, “Wewe Umechoka Sana?”, kwa ajili ya ibada, kuimba na kujifunza. Maneno ya Wimbo Wewe umechoka sana? Wataka raha? Kwake Yesu utapata furaha. Alama anazo yeye? Sasa! makovu ya mikono, na miguu, Na mbavu. Nacho kimivukwa taji Kichwa cha huba? Alivikwa taji kweli miiba. Huku nikimfuata nipate nini? Maonjo nje na ndani amani. Kwamba namwandama Bwana, Mwisho ni nini? Ni furaha na salama Mbinguni. ← Tenzi 52 | Tenzi Zote | Tenzi 54 → Tazama Tenzi za Rohoni 1–164 Omba App ya Tenzi za Rohoni kwa Android

Tenzi za Rohoni

Tenzi za Rohoni 52 – Yote Namtolea Yesu

Tenzi za Rohoni 52 – Yote Namtolea Yesu Tenzi Na. 52 Soma maneno kamili ya Tenzi za Rohoni namba 52, “Yote Namtolea Yesu”, kwa ajili ya ibada, kuimba na kujifunza. Maneno ya Wimbo Yote namtolea Yesu Nampa moyo wote, Nitampenda siku zote, Namwandama kila saa. Yote kwa Yesu, Yote kwa Yesu, Yote kwako, Ee mwokozi, Natoa sasa. Yote namtolea Yesu, Nainamia pake; Nimeacha na anasa, Kwako Yesu nipokee, Yote namtolea Yesu, Nifanye niwe wako; Nipe Roho yako, Bwana, Anilinde daima, Yote namtolea Yesu, Nami naona sasa; Furaha ya ukombozi, Nasifu jina lake, ← Tenzi 51 | Tenzi Zote | Tenzi 53 → Tazama Tenzi za Rohoni 1–164 Omba App ya Tenzi za Rohoni kwa Android

Tenzi za Rohoni

Tenzi za Rohoni 51 – Mungu Twatoa Shukrani

Tenzi za Rohoni 51 – Mungu Twatoa Shukrani Tenzi Na. 51 Soma maneno kamili ya Tenzi za Rohoni namba 51, “Mungu Twatoa Shukrani”, kwa ajili ya ibada, kuimba na kujifunza. Maneno ya Wimbo Bwana Yesu atakuja, Vumilia! Omba, ukiwa na haja, Vumilia! Mbingunu Mungu aliko, Mwamini Mwokozi wako, Nawe utafika huko, Vumilia! Ikikucheka dunia, Vumilia! Mwovu atakuvizia, Vumilia! Hataweza kukushinda, Bwana Yesu akulinda, Roho yako, akupenda, Vumilia! Na ukiwa hatarini, Vumilia! Dhiki nyingi duniani, Vumilia! Vyatupasa kuyakuta, Majaribu na matata, Na Bwana hakutuficha; Vumilia! Adui wakikutana, Vumilia! Na ndugu wakikukana, Vumilia! Zote, zote zitakwisha, Nguvu zote za kutisha Mungu chini atashusha; Vumilia! Moyoni una majonzi, Vumilia! Ndiyo bonde-ya-machozi, Vumilia! Hima tutaandamana, Kwetu Mbinguni na Bwana Tena hatutaachana; Vumilia! ← Tenzi 50 | Tenzi Zote | Tenzi 52 → Tazama Tenzi za Rohoni 1–164 Omba App ya Tenzi za Rohoni kwa Android

Tenzi za Rohoni

Tenzi za Rohoni 50 – Yesu Nakupenda, U Mali Yangu

Tenzi za Rohoni 50 – Yesu Nakupenda, U Mali Yangu Tenzi Na. 50 Soma maneno kamili ya Tenzi za Rohoni namba 50, “Yesu Nakupenda, U Mali Yangu”, kwa ajili ya ibada, kuimba na kujifunza. Maneno ya Wimbo Yesu nakupenda, U mali yangu, Anasa za dhambi sitaki kwangu; Na Mwokozi aliyeniokoa, Sasa nakupenda, kuzidi pia. Moyo umejaa mapenzi tele Kwa vile ulivyonipenda mbele, Uhai wako ukanitolea Sasa nakupenda, kuzidi pia. Ulipoangikwa Msalabani Tusamehewe tulio dhambini; Taji ya miiba uliyoivaa, Sasa nakupenda, kuzidi pia. Niwapo hai, niwapo maiti, Kupendana nawe kamwe siachi; Hari za kifo zikinienea, Sasa nakupenda, kuzidi pia. Mawanda mazuri, na masikani Niyatazamapo huko Mbinguni, Tasema na taji nitakayovaa Sasa nakupenda, kuzidi pia. ← Tenzi 49 | Tenzi Zote | Tenzi 51 → Tazama Tenzi za Rohoni 1–164 Omba App ya Tenzi za Rohoni kwa Android

Tenzi za Rohoni

Tenzi za Rohoni 49 – Nitwae Hivi Nilivyo

Tenzi za Rohoni 49 – Nitwae Hivi Nilivyo Tenzi Na. 49 Soma maneno kamili ya Tenzi za Rohoni namba 49, “Nitwae Hivi Nilivyo”, kwa ajili ya ibada, kuimba na kujifunza. Maneno ya Wimbo Nitwae hivi nilivyo, Umemwaga damu yako, Nawe ulivyoniita, Bwana Yesu,naja,naja. Hivi nilivyo;si langu Kujiosha roho yangu; Nisamehe dhambi zangu, Bwana Yesu,naja,naja. Hivi nilivyo; sioni Kamwe furaha moyoni; Daima ni mashakani, Bwana Yesu,naja,naja. Hivi nilivyo kipofu, maskini na mpungufu; Wewe u mtimilifu; Bwana Yesu,naja,naja. Nawe hivi utanitwaa; Nisithubutu kukawa, Na wewe hutanikataa, Bwana Yesu,naja,naja. Hivi nilivyo;mapenzi Yamenipa njia wazi; Hali na mali sisazi, Bwana Yesu,naja,naja. ← Tenzi 48 | Tenzi Zote | Tenzi 50 → Tazama Tenzi za Rohoni 1–164 Omba App ya Tenzi za Rohoni kwa Android

Tenzi za Rohoni

Tenzi za Rohoni 48 – Naweka Dhambi Zangu

Tenzi za Rohoni 48 – Naweka Dhambi Zangu Tenzi Na. 48 Soma maneno kamili ya Tenzi za Rohoni namba 48, “Naweka Dhambi Zangu”, kwa ajili ya ibada, kuimba na kujifunza. Maneno ya Wimbo Naweka dhambi zangu Juu yake Bwana Kuziondoa, kwangu Hulemea sana; Na uaili wangu Ameuondoa; Dawa yangu ni damu, Kwa hiyo napoa. Na uhitaji wangu Nitamjuvisha Kwa upungufu wangu Yeye anatosha; Majonzi yangu yote Na mizigo yangu, Atachukua vyote Yesu Bwana wangu. Na roho yangu nayo, Imechoka sana; Namletea hiyo Ilindwe na Bwana; Ni jema jina lake, Nalo lapendeza, Imanweli na kwake tutalitukuza. Natamani daima Niwe kama Bwana, Mpole, tena mwema, Wa mapenzi sana; Zaidi natamani Kwenda kwake juu, Nikaone mbinguni Enzi yake kuu. ← Tenzi 47 | Tenzi Zote | Tenzi 49 → Tazama Tenzi za Rohoni 1–164 Omba App ya Tenzi za Rohoni kwa Android

Tenzi za Rohoni

Tenzi za Rohoni 47 – Ni WaKo Wewe

Tenzi za Rohoni 47 – Ni WaKo Wewe Tenzi Na. 47 Soma maneno kamili ya Tenzi za Rohoni namba 47, “Ni WaKo Wewe”, kwa ajili ya ibada, kuimba na kujifunza. Maneno ya Wimbo Ni wako wewe, nimekujua, Na umeniambia; Lakini Bwana, nataka kwako nizidi kusongea. Bwana vuta, vuta, nije nisongee, Sana, kwako mtini. Bwana vuta, vuta, nije nisongee, Pia damu ya thamani. Niweke sasa nikatumike Kwa nguvu za neema; Uyapendayo nami nipende, Nizidi kukwandama. Nina furaha tele kila saa Nizungumzavyo kwako, Nikuombapo nami napata kujua nia yako. Mapenzi yako hayapimiki, Ila ng’ambo ya liko. Anasa pia sitazijua, Bila kufika kwako. ← Tenzi 46 | Tenzi Zote | Tenzi 48 → Tazama Tenzi za Rohoni 1–164 Omba App ya Tenzi za Rohoni kwa Android

Tenzi za Rohoni

Tenzi za Rohoni 46 – Twae Wangu Uzima

Tenzi za Rohoni 46 – Twae Wangu Uzima Tenzi Na. 46 Soma maneno kamili ya Tenzi za Rohoni namba 46, “Twae Wangu Uzima”, kwa ajili ya ibada, kuimba na kujifunza. Maneno ya Wimbo Twae wangu uzima, Sadaka ya daima; Twae saa na siku, Zikutukuze huku. Twae mikono nayo Ifanye upendavyo, Twae yangu miguu Kwa wongozi wako tu. Twae sauti yangu, Niimbe kwa Mungu tu; Itwae na midomo, Ijae neno lako. Twae dhanabu pia, Na yote ya dunia; Twae yangu hekima, Upendavyo tumia. Nia itwae, Mungu, Haitakuwa yangu; Twae moyo; ni wako, Uwe makazi yako. Twae mapenzi yangu, Sifa za moyo wangu; Twae kabisa nafsi Nniwe wako halisi. ← Tenzi 45 | Tenzi Zote | Tenzi 47 → Tazama Tenzi za Rohoni 1–164 Omba App ya Tenzi za Rohoni kwa Android

banner
Scroll to Top