Tenzi za Rohoni 54 – Yesu Nataka Kutakaswa Sana

Tenzi za Rohoni 54 – Yesu Nataka Kutakaswa Sana

Tenzi Na. 54

Soma maneno kamili ya Tenzi za Rohoni namba 54, “Yesu Nataka Kutakaswa Sana”, kwa ajili ya ibada, kuimba na kujifunza.


Maneno ya Wimbo

Yesu nataka kutakaswa sana,
Nataka moyo uwe enzi yako.
Ukiangushe kilichoinuka
Unioshe sasa niwe mweupe.
Mweupe tu, ndiyo mweupe,
Ukiniosha nitakuwa safi.
Bwaba Yesu, unitazame sasa,
Unifanye niwe dhabihu hai;
Najitoa kwako, na moyo wote;
Unioshe sasa niwe mweupe.
Bwana kwa hiyo nakuomba sana,
Nakungojea miguuni pako,
Naomba unioshe damuni tu,
Unioshe sasa niwe mweupe.
Bwana nidumu kukungojea,
Niumbie moyo safi, Ee Mungu,
Wanaokujia hutupi kamwe,
Unioshe sasa niwe mweupe.


Tazama Tenzi za Rohoni 1–164


Omba App ya Tenzi za Rohoni kwa Android

banner
Scroll to Top