Tenzi za Rohoni 59 – Peleleza Ndani Yangu

Tenzi za Rohoni 59 – Peleleza Ndani Yangu

Tenzi Na. 59

Soma maneno kamili ya Tenzi za Rohoni namba 59, “Peleleza Ndani Yangu”, kwa ajili ya ibada, kuimba na kujifunza.


Maneno ya Wimbo

Peleleza ndani yangu,
Iwe safi nia,
Kwangu kama kwako Mungu,
Idhihiri pia.
Peleleza moyo wangu
Uunifunulie,
Yaliyomo ndani yangu
Nami niyajue.
Kwanza washe zako tambi,
Kumefunga giza;
Nijue ambavyo dhambi
Ni la kuchukiza.
Peleleza na mawazo
Ni mbegu za mambo,
Asili ya machukizo,
Maumbuo – umbo.
Zidi kuyapeleleza
Katikati yangu
Hata wishe nifundisha
Udhaifu wangu.
Hapo nikikwinamia
Mbele zako, Mungu,
Hakika nitakujua
U mpenzi wangu.


Tazama Tenzi za Rohoni 1–164


Omba App ya Tenzi za Rohoni kwa Android

banner
Scroll to Top