Tenzi za Rohoni 56 – Ni siku kuu siku ile

Tenzi za Rohoni 56 – Ni siku kuu siku ile

Tenzi Na. 56

Soma maneno kamili ya Tenzi za Rohoni namba 56, “Ni siku kuu siku ile”, kwa ajili ya ibada, kuimba na kujifunza.


Maneno ya Wimbo

Ni siku kuu siku ile
Ya kumkiri Mwokozi!
Moyo umejaa tele,
Kunyamaza hauwezi.
Siku kuu! Siku kuu!
Ya kuoshwa dambi zangu kuu!
Hukesha na kuomba tu,
Ananiongoza miguu.
Siku kuu! siku kuu!
Ya kuoshwa dhambi zangu kuu.
Tumekwisha kupatana
Mimi wake, yeye wangu,
Na sasa nitamwandama,
Nikiri neno la Mungu.
Moyo tulia kwa Bwana
Kiini cha raha yako,
Huna njia mbili tena;
Yesu ndiye njia yako.
Nadhiri yangu ya mbele
Nitaiweka daima,
Hata ije siku ile,
Ya kwonana kwa salama


Tazama Tenzi za Rohoni 1–164


Omba App ya Tenzi za Rohoni kwa Android

banner
Scroll to Top