Tenzi za Rohoni 75 – Waimba, Sikizeni

Tenzi za Rohoni 75 – Waimba, Sikizeni

Tenzi Na. 75

Soma maneno kamili ya Tenzi za Rohoni namba 75, “Waimba, Sikizeni”, kwa ajili ya ibada, kuimba na kujifunza.


Maneno ya Wimbo

Waimba, sikizeni,
Malaika Mbinguni;
Wimbo wa tamu sana
Wa pendo zake Bwana,
“Duniani salama,
Kwa wakosa rehema.”
Sisi sote na twimbe
Nao wale wajumbe;
Waimba, sikizeni,
Malaika mbinguni.
Ndiye Bwana wa Mbingu,
Tangu milele Mungu,
Amezaliwa mwili,
Mwana wa mwanamwali;
Ametoka enzini
Kuja ulimwenguni
Mwokozi atufie,
Ili tusipotee.
Waimba, sikizeni,
Malaika Mbinguni.
Mtukufu wa amani
Ametoka Mbinguni,
Jua la haki, ndiye
Atumulikiaye;
Amejivua enzi,
Alivyo na mapenzi,
Ataka kutuponya,
Kutuzalisha upya,
Waimba sikizeni,
Malaika Mbinguni.
Njoo upesi, Bwana,
Twakutamani sana;
Kaa nasi, mwokozi
Vita hatuviwezi;
Vunja kichwa cha nyoka,
Sura zako andika,
Tufanane na wewe,
Kwetu sifa upewe,
Waimba, sikizeni,
Malaika Mbinguni.


Tazama Tenzi za Rohoni 1–164


Omba App ya Tenzi za Rohoni kwa Android

banner
Scroll to Top