Tenzi za Rohoni 95 – Hivi vita, vimekoma
Tenzi za Rohoni 95 – Hivi vita, vimekoma Tenzi Na. 95 Soma maneno kamili ya Tenzi za Rohoni namba 95, “Hivi vita, vimekoma”, kwa ajili ya ibada, kuimba na kujifunza. Maneno ya Wimbo Aleluya! Aleluya! Aleluya! Hivi vita vimekoma, Vimeshindwa na uzima, Na asifiwe daima, Bwana Yesu. Nguvu za kifo ni hizo, Ila hazina uwezo, Ndizo sasa avunjazo, Bwana Yesu. Siku tatu za huzuni, Kisha atoka ufuni, Asifiwe duniani, Bwana Yesu. Mapingu ameyavunja, Mbingu amezifungua, Nasi sasa twamwimbia, Bwana Yesu. Na ulivyopigwa wewe, Ni kwamba tufunguliwe, Milele na usifiwe, Bwana Yesu. ← Tenzi 94 | Tenzi Zote | Tenzi 96 → Tazama Tenzi za Rohoni 1–164 Omba App ya Tenzi za Rohoni kwa Android