Tenzi za Rohoni 89 – Kwa Kalvari

Tenzi za Rohoni 89 – Kwa Kalvari

Tenzi Na. 89

Soma maneno kamili ya Tenzi za Rohoni namba 89, “Kwa Kalvari”, kwa ajili ya ibada, kuimba na kujifunza.


Maneno ya Wimbo

Muda mwingi nilipotea,
Sikufahamu msalaba,
Wala aliyenifilia,
Kwa Kalvari.
Rehema bure na neema,
Samaha nalo nilipewa,
Ndipo aliponifungua
Kwa Kalvari.
Kwa neno lake Bwana Mungu,
Nilijiona mimi mwovu,
Nikageuka na kutubu,
Kwa Kalvari.
Yote kwa Yesu namtolea,
Ndiye mfalme wa pekee sasa,
Kwa furaha nitamwimbia,
Wa Kalvari.
Jinsi pendo lilivyo kuu,
Neema ilishuswa toka juu,
Alitufanyia wokovu
Kwa Kalvari.


Tazama Tenzi za Rohoni 1–164


Omba App ya Tenzi za Rohoni kwa Android

banner
Scroll to Top