Tenzi za Rohoni 88 – Ndiyo Damu ya Baraka

Tenzi za Rohoni 88 – Ndiyo Damu ya Baraka

Tenzi Na. 88

Soma maneno kamili ya Tenzi za Rohoni namba 88, “Ndiyo Damu ya Baraka”, kwa ajili ya ibada, kuimba na kujifunza.


Maneno ya Wimbo

Ndiyo damu ya baraka ituoshayo wakosa,
Kwake Bwana twaokoka, nasi twamsifu sasa;
Nimestahili hukumu, siwezi kujitakasa;
Nioshe katika damu, takuwa safi kabisa.
Safi kabisa; safi kabisa!
Nioshe katika damu;
Takuwa safi kabisa.
Yesu alivikwa miiba, na kuangikwa Mtini,
Na maumivu si haba yaliyompata chini.
Nataka kijito hicho niende kuoga sasa;
Ndicho kinitakasacho, nami ni safi kabisa.
Safi kabisa; safi kabisa!
Ndicho kinitakasacho,
Nami ni safi kabisa.
Baba, kweli nimekosa, moyo wangu ni dhaifu;
Dhambi ni nyingi kabisa, nipate wapi wokovu?
Yesu kijitoni pako, naja naamini sasa;
Nioshe kwa damu yako, takuwa safi kabisa.
Safi kabisa; safi kabisa!
Nioshe kwa damu yako,
Nami ni safi kabisa.


Tazama Tenzi za Rohoni 1–164


Omba App ya Tenzi za Rohoni kwa Android

banner
Scroll to Top