Skip to main content

Author name: contact@devinevisiontech.com

Tenzi za Rohoni

Tenzi za Rohoni 105 – Kuwatafuta

Tenzi za Rohoni 105 – Kuwatafuta Tenzi Na. 105 Soma maneno kamili ya Tenzi za Rohoni namba 105, “Kuwatafuta”, kwa ajili ya ibada, kuimba na kujifunza. Maneno ya Wimbo Kuwatafuta wasioweza, Kuomba wamrejee Yesu, Kuwaambia maneno yake, “Njooni kwangu, nawapenda”. Nitakwenda, (kwenda), niwatafute Waongofu (wa Bwana) wageuke, Waingie (wote) katika zizi La Mkombozi (wetu) Yesu kristo. Kuwatafuta wasioweza, Waonyeshwe Mwokozi wetu, Kuwaongoza, wapate wote Uzima wa milele. Kazi hiyo nataka kufanya, Leo nimesikia mwito Kuwainua waangukao, Waletwe kwake Yesu njia. ← Tenzi 104 | Tenzi Zote | Tenzi 106 → Tazama Tenzi za Rohoni 1–164 Omba App ya Tenzi za Rohoni kwa Android

Tenzi za Rohoni

Tenzi za Rohoni 104 – Twasoma Ni Njema Sana

Tenzi za Rohoni 104 – Twasoma Ni Njema Sana Tenzi Na. 104 Soma maneno kamili ya Tenzi za Rohoni namba 104, “Twasoma Ni Njema Sana”, kwa ajili ya ibada, kuimba na kujifunza. Maneno ya Wimbo Twasoma, ni njema sana Mbinguni, kwa Bwana; Twasoma, dhambi hapana, Mbinguni kwa Bwana; Malaika wema wako, Vinanda vizuri viko, Na majumba tele yako, Mbinguni kwa Bwana. Siku zote ni mchana, Ni nchi ya raha; Wala machozi hapana, Ni nchi ya raha; Walioko wanuona Uso wa Mwokozi, tena Jua jingine hapana, Ni nchi ya raha. Nyama na vitu viovu Havimo kabisa; Kifo nacho, na ubovu, Havimo kabisa. Ni watakatifu wote, Wameoshwa dhambi zote; Wasiosafiwa wote Hawamo kabisa. Tuna dhambi, pia sote, Mwokozi akafa; Kwake tutaoshwa zote, Mwokozi akafa; Kwake twapata wokovu, Tutawona utukufu; Mbinguni tutamsifu; Mwokozi akafa. Baba, mama, ndugu zetu, Twendeni kwa Bwana; Huku chini sio kwetu, Twendeni kwa Bwana; Tusishikwe na dunia, Na dhambi kutulemea; Tutupe vya chini pia, Twendeni kwa Bwana. ← Tenzi 103 | Tenzi Zote | Tenzi 105 → Tazama Tenzi za Rohoni 1–164 Omba App ya Tenzi za Rohoni kwa Android

Tenzi za Rohoni

Tenzi za Rohoni 103 – Kaa Nami

Tenzi za Rohoni 103 – Kaa Nami Tenzi Na. 103 Soma maneno kamili ya Tenzi za Rohoni namba 103, “Kaa Nami”, kwa ajili ya ibada, kuimba na kujifunza. Maneno ya Wimbo Kaa nami, ni usiku tena; Usiniache gizani, Bwana; Msaada wako haukomi; Nili peke yangu, kaa nami. Siku zetu hazikawi kwisha, Sioni la kunifurahisha; Hakuna ambacho hakikomi, Usiye na mwisho kaa nami. Nina haja nawe kila saa; Sina mwingine wa kunifaa; Mimi nitaongozwa na nani Ila wewe? Bwana, kaa name. Sichi neno uwapo karibu; Nipatalo lote, si taabu; Kifo na kaburi haviumi; Nitashinda kwako, kaa nami. Nilalapo nikuone wewe, Gizani mote nimulikiwe; Nuru za mbinguni hazikomi, Siku zangu zote kaa nami. ← Tenzi 102 | Tenzi Zote | Tenzi 104 → Tazama Tenzi za Rohoni 1–164 Omba App ya Tenzi za Rohoni kwa Android

Tenzi za Rohoni

Tenzi za Rohoni 102 – Kazi Yangu Ikiisha

Tenzi za Rohoni 102 – Kazi Yangu Ikiisha Tenzi Na. 102 Soma maneno kamili ya Tenzi za Rohoni namba 102, “Kazi Yangu Ikiisha”, kwa ajili ya ibada, kuimba na kujifunza. Maneno ya Wimbo Kazi yangu ikiisha, nami nikiokoka; Na kuvaa kutokuharibika, Nitamjua Mwokozi nifikapo ng’amboni; Atakuwa wa kwanza kunilaki. Nitamjua, nitamjua, nikimwona uso kwa uso; Nitamjua, nitamjua, kwa alama za misumari. Furaha nitapata nikiona makao Bwana aliyotuandalia; Nitamsifu mwokozi kwa rehema na pendo Vilivyonipa pahali Mbinguni. Nao waliokufa katika Bwana Yesu, Nitawaona tena huko juu; Lakini nifikapo kwake huko Mbinguni, Nataka kumwona Mwokozi kwanza. Milangoni mwa mji Bwana atanipitisha, Pasipo machozi wala huzuni. Nitauimba wimbo wa milele; lakini Nataka kumwona Mwokozi kwanza. ← Tenzi 101 | Tenzi Zote | Tenzi 103 → Tazama Tenzi za Rohoni 1–164 Omba App ya Tenzi za Rohoni kwa Android

Tenzi za Rohoni

Tenzi za Rohoni 101 – Twonane Milele

Tenzi za Rohoni 101 – Twonane Milele Tenzi Na. 101 Soma maneno kamili ya Tenzi za Rohoni namba 101, “Twonane Milele”, kwa ajili ya ibada, kuimba na kujifunza. Maneno ya Wimbo Nyimbo na tuziimbe tena Za alivyotupenda mbele; Kwa damu ya thamani sana! Mbinguni twonane milele. Twonane milele, Twonane bandarini kule; Twonane milele, Twonane bandarini kule. Hupozwa kila aoshwaye, Kwa damu ya Kondoo yule; Ataishi afurahiye Vya Yesu mbinguni milele. Hata sasa hufurahia Tamu yake mapenzi yale, Je, kwake tukifikilia, Kutofarakana milele? Twende mbele kwa jina lake, Hata aje mwokozi yule, Atatukaribisha kwake, Tutawale naye milele. Sauti zetu tuinue Kumsifu Mwokozi yule, Ili watu wote wajue Wokovu u kwake milele. ← Tenzi 100 | Tenzi Zote | Tenzi 102 → Tazama Tenzi za Rohoni 1–164 Omba App ya Tenzi za Rohoni kwa Android

Tenzi za Rohoni

Tenzi za Rohoni 100 – Tumrudie Bwana

Tenzi za Rohoni 100 – Tumrudie Bwana Tenzi Na. 100 Soma maneno kamili ya Tenzi za Rohoni namba 100, “Tumrudie Bwana”, kwa ajili ya ibada, kuimba na kujifunza. Maneno ya Wimbo Mbona washangaa njiani? Mbona warejea nyuma? Warudi tena gizani Alimokutoa Bwana? Ni ya bure yote haya, Uliyofunzwa ya Mungu? Ni bure amekufia Bwana Yesu kwa uchungu? Wamtia kristo aibu Na maneno yake pia? Siku yaja ya hesabu, Utamjibuje Bwana? Upandapo tena hayo, Halafu utayavuna. Rudi kwa Bwana upesi, Mwombe akupokee tena. ← Tenzi 99 | Tenzi Zote | Tenzi 101 → Tazama Tenzi za Rohoni 1–164 Omba App ya Tenzi za Rohoni kwa Android

Tenzi za Rohoni

Tenzi za Rohoni 99 – Maelfu Na Maelfu

Tenzi za Rohoni 99 – Maelfu Na Maelfu Tenzi Na. 99 Soma maneno kamili ya Tenzi za Rohoni namba 99, “Maelfu Na Maelfu”, kwa ajili ya ibada, kuimba na kujifunza. Maneno ya Wimbo Maelfu na maelfu Wenye nguo bora! Masafu ya waongofu Wenye na bendera! Amekwisha kamili Vita vya shetani Fungueni lango hili; Njoni, ingieni! Imbeni aleluya, Zipae Mbinguni! Pigeni sana sauti Kwa kutumaini! Kwa hiyo viliumbwa Nchi hata Mbingu Dhiki za muda zikisha, Asifiwe Yesu. Loo! Tukionana Pwani ya ng’amboni! Loo! Tukishirikiana Milele Mbinguni! Midomo yote pia, Huko itaimba Wajane kufufukiwa Na kila yatima! Himiza enzi yako, Uliyetufia Utimize watu wako, Wakosaji pia, Mpendwa wa taifa twakutumaini! Uzifunue ishara Urudi enzini! ← Tenzi 98 | Tenzi Zote | Tenzi 100 → Tazama Tenzi za Rohoni 1–164 Omba App ya Tenzi za Rohoni kwa Android

Tenzi za Rohoni

Tenzi za Rohoni 98 – Huyo Ndiye! Anashuka

Tenzi za Rohoni 98 – Huyo Ndiye! Anashuka Tenzi Na. 98 Soma maneno kamili ya Tenzi za Rohoni namba 98, “Huyo Ndiye! Anashuka”, kwa ajili ya ibada, kuimba na kujifunza. Maneno ya Wimbo Huyo ndiye! anaskuka, Aliyetufilia, Wengi waliookoka, Wakimfurahia, Aleluya! Yesu aturudia. Sote tutamtazama, Amekaa kitini, Nao waliomcoma, Kumkaza mtini, Na kilio, wamuone enzini. Alama za kifo chake Hata sasa anazo Na waaminifu wake Wapendezewa nazo. Alipata, Kwetu alama hizo. Wokovu utakiwao Sasa wapatikana, Na watakatifu hao Mbinguni wakutana Kumlaki, Ndiyo siku ya Bwana Wakusujudie wote Mbele ya kiti chako. Zako, Bwana, nguvu zote Itwae milki yako Njoo Bwana, Sisi tu watu wako. ← Tenzi 97 | Tenzi Zote | Tenzi 99 → Tazama Tenzi za Rohoni 1–164 Omba App ya Tenzi za Rohoni kwa Android

Tenzi za Rohoni

Tenzi za Rohoni 97 – Tazameni Huyo Ndiye

Tenzi za Rohoni 97 – Tazameni Huyo Ndiye Tenzi Na. 97 Soma maneno kamili ya Tenzi za Rohoni namba 97, “Tazameni Huyo Ndiye”, kwa ajili ya ibada, kuimba na kujifunza. Maneno ya Wimbo Tazameni huyo ndiye, Mwenye kushinda vita; Haya, tumsujudie; Nyara anazileta; Watu wote msifuni, Sasa yumo kitini. Msifuni malaika, Mtukuzeni sana, Wote waliookoka Watamsifu Bwana; Watu wote msifuni, Sasa yumo kitini. Walimfanya dhihaka Zamani wenye shari, Kwao waliookoka Ni Bwana wa fahari; Watu wote msifuni. Sasa yumo Kitini. Nyimbo nzuri, sikizeni, Ni nyimbo za sifa kuu, Za Bwana Yesu kitini, Kutawazwa, yeye tu; Watu wote msifuni Sasa yumo Kitini. ← Tenzi 96 | Tenzi Zote | Tenzi 98 → Tazama Tenzi za Rohoni 1–164 Omba App ya Tenzi za Rohoni kwa Android

Tenzi za Rohoni

Tenzi za Rohoni 96 – Mle kaburini, Yesu Mwokozi!

Tenzi za Rohoni 96 – Mle kaburini, Yesu Mwokozi! Tenzi Na. 96 Soma maneno kamili ya Tenzi za Rohoni namba 96, “Mle kaburini, Yesu Mwokozi!”, kwa ajili ya ibada, kuimba na kujifunza. Maneno ya Wimbo Mle kaburini, Yesu Mwokozi! Alilazwa chini, Bwana wangu! Bwana! Amefufuka, Kifo kimeshindwa kabisa! Gizani mle alitoka chini, Sasa atawala huko Mbinguni! Yu hai! Yu hai! Bwana Yesu yu hai! Aungoja huo, Yesu Mwokozi! Mchana ujao, Bwana wangu! Walinda kaburi, Yesu Mwokozi! Bure ni muhuri, Bwana wangu! Kifo kimeshindwa, Yesu mwokozi! Pingu zimevunjwa, Bwana wangu! ← Tenzi 95 | Tenzi Zote | Tenzi 97 → Tazama Tenzi za Rohoni 1–164 Omba App ya Tenzi za Rohoni kwa Android

banner
Scroll to Top