Tenzi za Rohoni 115 – Kilima kando Ya Mji
Tenzi za Rohoni 115 – Kilima kando Ya Mji Tenzi Na. 115 Soma maneno kamili ya Tenzi za Rohoni namba 115, “Kilima kando Ya Mji”, kwa ajili ya ibada, kuimba na kujifunza. Maneno ya Wimbo Kilima kando ya mji Alikufa Bwana; Kuokoa wakosaji Akateswa sana. Kabisa hayasemeki, Mateso dhaifu Alikufa mwenye Haki Tupate wokovu. Alimwaga damu yake Ili tuwe wema, Tufae kukaa kwake Mbinguni daima. Hatuna mwenye imani Aliye na haki, Wa kutosha yetu deni, Rafiki Yesu tu. Alijua peke yake Kufungu Mbingu Ufunguo damu yake Kondoo wa Mungu. Aliyetupenda hivyo Nasi tumpende, Tukamtumai vivyo Na kazi tutende. ← Tenzi 114 | Tenzi Zote | Tenzi 116 → Tazama Tenzi za Rohoni 1–164 Omba App ya Tenzi za Rohoni kwa Android