Tenzi za Rohoni 114 – Bwana Mungu, Nashangaa Kabisa
Tenzi Na. 114
Soma maneno kamili ya Tenzi za Rohoni namba 114, “Bwana Mungu, Nashangaa Kabisa”, kwa ajili ya ibada, kuimba na kujifunza.
Maneno ya Wimbo
Bwana Mungu, nashangaa kabisa
Nikitazama kama vilivyo
Nyota, ngurumo, vitu vingi vyote
viumbwavyo kwa uwezo wako.
Roho yangu na ikuimbie
Jinsi Wewe ulivyo Mkuu,
Roho yangu na ikuimbie
Jinsi Wewe ulivyo Mkuu.
Nikitembea pote duniani,
Ndege huimba, nawasikia,
Milima hupendeza macho sana,
Upepo nao nafurahia.
Nikikumbuka kama Wewe Mungu
Ulivyompeleka Mwanao,
Afe azichukue dhambi zetu,
Kuyatambua ni vigumu mno.
Yesu Mwokozi utakaporudi
Kunichukua kwenda Mbinguni,
Nitashukuru na kwimba milele,
Wote wajue jinsi ulivyo.