Tenzi za Rohoni 107 – Ewe,Baba Wa Mbinguni
Tenzi Na. 107
Soma maneno kamili ya Tenzi za Rohoni namba 107, “Ewe,Baba Wa Mbinguni”, kwa ajili ya ibada, kuimba na kujifunza.
Maneno ya Wimbo
Ewe, Baba wa Mbinguni,
Usikie twombalo
Hapa chini duniani,
Na uwe radhi nalo
Ee Mungu, bariki
Ndugu hawa wawili!
Ee Mungu, bariki
Ndugu hawa wawili!
Watu hawa mbele zako,
Na mbele ya kanisa;
Watimize Neno lako
Wanakutana sasa.
Kama Yesu na Kanisa,
Ni mmoja, na hivyo,
Watu hawawape sasa
Wawe mmoja vivyo
Walinde, Bwana, daima,
Wabariki nyumbani
Uwape nyingi salama
Humu ulimwenguni.
Wabariki, ewe Bwana,
Watu hawa wawili,
Wape upaji wa wana,
Wafurahishwe kweli.
Siku za duniani
Zitakapopungua,
Wape kurithi Mbinguni
Mema ya kwendelea.