Tenzi za Rohoni 97 – Tazameni Huyo Ndiye
Tenzi Na. 97
Soma maneno kamili ya Tenzi za Rohoni namba 97, “Tazameni Huyo Ndiye”, kwa ajili ya ibada, kuimba na kujifunza.
Maneno ya Wimbo
Tazameni huyo ndiye,
Mwenye kushinda vita;
Haya, tumsujudie;
Nyara anazileta;
Watu wote msifuni,
Sasa yumo kitini.
Msifuni malaika,
Mtukuzeni sana,
Wote waliookoka
Watamsifu Bwana;
Watu wote msifuni,
Sasa yumo kitini.
Walimfanya dhihaka
Zamani wenye shari,
Kwao waliookoka
Ni Bwana wa fahari;
Watu wote msifuni.
Sasa yumo Kitini.
Nyimbo nzuri, sikizeni,
Ni nyimbo za sifa kuu,
Za Bwana Yesu kitini,
Kutawazwa, yeye tu;
Watu wote msifuni
Sasa yumo Kitini.