Tenzi za Rohoni 116 – Bwana U Sehemu Yangu
Tenzi Na. 116
Soma maneno kamili ya Tenzi za Rohoni namba 116, “Bwana U Sehemu Yangu”, kwa ajili ya ibada, kuimba na kujifunza.
Maneno ya Wimbo
Bwana u sehemu yangu, rafiki yangu wewe;
Katika safari yangu, tatembea na wewe;
Pamoja na wewe, pamoja na wewe,
katika safari yangu, tatembea na wewe.
Mali hapa sikutaka, ili niheshimiwe,
na yanikute mashaka, sawa sawa na wewe.
Pamoja na wewe, pamoja na wewe,
heri nikute mashaka sawasawa na wewe.
Niongoze safarini, mbele unichukue,
mlangoni kwa mbinguni, niingie na wewe.
Pamoja na wewe, pamoja na wewe,
mlangoni kwa mbinguni, niingie na wewe.