Tenzi za Rohoni 117 – Tufani Inapovuma
Tenzi Na. 117
Soma maneno kamili ya Tenzi za Rohoni namba 117, “Tufani Inapovuma”, kwa ajili ya ibada, kuimba na kujifunza.
Maneno ya Wimbo
Tufani inapovuma
Sana moyoni mwangu,
Huona pa kujificha
Mkononi mwa Mungu.
Hunificha, hunificha
Adui hatanipata,
Hunificha, hunificha,
Mkononi mwake.
Pengine kuna taabu
Yanisongeza kwake;
Naijua si hasira,
Ni ya mapenzi yake.
Adui wakiniudhi
Nami nikisumbuka,
Mungu atavigeuza
Vyote viwe baraka.
Niishipo duniani
Ni tufani daima,
Anilindapo rohoni
Nitakaa salama.