Tenzi za Rohoni 111 – Neno,Lako Bwana
Tenzi Na. 111
Soma maneno kamili ya Tenzi za Rohoni namba 111, “Neno,Lako Bwana”, kwa ajili ya ibada, kuimba na kujifunza.
Maneno ya Wimbo
Neno lako, Bwana,
Ni imara sana;
Lilo latwongoza,
Lilo latufunza.
Adui wabaya
Wakikaribia,
Neno lake Bwana
Ni ulinzi sana.
Siku za dhoruba
Soma ukiomba;
Neno lake Bwana
Msaada sana.
Ukiliamini,
Hwenda na amani;
Una na furaha
Neno ni siraha.
Ni furaha kweli,
Na wingi wa mali,
Neno lake Bwana
Kwa wasiokana
Neno la rehema,
Tukali wazima;
Faraja I papo,
Tufarikanapo.