Tenzi za Rohoni 96 – Mle kaburini, Yesu Mwokozi!
Tenzi Na. 96
Soma maneno kamili ya Tenzi za Rohoni namba 96, “Mle kaburini, Yesu Mwokozi!”, kwa ajili ya ibada, kuimba na kujifunza.
Maneno ya Wimbo
Mle kaburini, Yesu Mwokozi!
Alilazwa chini, Bwana wangu!
Bwana! Amefufuka,
Kifo kimeshindwa kabisa!
Gizani mle alitoka chini,
Sasa atawala huko Mbinguni!
Yu hai! Yu hai!
Bwana Yesu yu hai!
Aungoja huo, Yesu Mwokozi!
Mchana ujao, Bwana wangu!
Walinda kaburi, Yesu Mwokozi!
Bure ni muhuri, Bwana wangu!
Kifo kimeshindwa, Yesu mwokozi!
Pingu zimevunjwa, Bwana wangu!