Tenzi za Rohoni 87 – Deni Ya Dhambi Ilimalizika
Tenzi Na. 87
Soma maneno kamili ya Tenzi za Rohoni namba 87, “Deni Ya Dhambi Ilimalizika”, kwa ajili ya ibada, kuimba na kujifunza.
Maneno ya Wimbo
Deni yangu ya dhambi,
Yesu amelipa.
Kwake msalabani
Nilipewa uzima.
Deni ya dhambi,
Msalabani,
Ilimalizikia,
Ni huru kabisa.
Bwana Yesu asema,
“Mwanangu dhaifu,
Uwezo wa ushindi
Hupatikana kwangu.”
Bwana, kweli naona,
Nguvu zako pekee
Huondoa ukoma,
Niwe kipya kiumbe.
Sina wema moyoni,
Nidai neema,
Nakubali kabisa,
Kwa damu kusafiwa.
Hata huko Mbinguni
Miguuni pake,
“Yesu alinifia,”
Nitaimba milele.