Tenzi za Rohoni 60 – Waponyeni Watu
Tenzi Na. 60
Soma maneno kamili ya Tenzi za Rohoni namba 60, “Waponyeni Watu”, kwa ajili ya ibada, kuimba na kujifunza.
Maneno ya Wimbo
Waponyeni watu wamo kifoni,
Watoeni walio shimoni;
Na aangukaye mumzuie;
Ya Bwana Yesu wahubirini.
Walio kifoni waokoeni,
Mwokozi yuko, wahubirini.
Wajapokawia anangojea,
Awasubiri waje tobani;
Msiwadharau, muwaonyeni;
Huwasamehe; wakiamini.
Myoyoni mwa ndani, yule shetani
Ameyaseta mawazo yao;
Lakini kwa Bwana huwa mazima,
Tukiwavuta kwa pole hao.
Kawaokoeni, wale njiani,
Mutimize mapenzi ya Bwana;
Na kwa nguvu zake warudi kwake,
Kwa subira waonyeni sana.