Tenzi za Rohoni 53 – Wewe Umechoka Sana?
Tenzi Na. 53
Soma maneno kamili ya Tenzi za Rohoni namba 53, “Wewe Umechoka Sana?”, kwa ajili ya ibada, kuimba na kujifunza.
Maneno ya Wimbo
Wewe umechoka sana?
Wataka raha?
Kwake Yesu utapata furaha.
Alama anazo yeye?
Sasa! makovu ya mikono, na miguu,
Na mbavu.
Nacho kimivukwa taji
Kichwa cha huba?
Alivikwa taji kweli miiba.
Huku nikimfuata nipate nini?
Maonjo nje na ndani amani.
Kwamba namwandama Bwana,
Mwisho ni nini?
Ni furaha na salama
Mbinguni.