Tenzi za Rohoni 52 – Yote Namtolea Yesu
Tenzi Na. 52
Soma maneno kamili ya Tenzi za Rohoni namba 52, “Yote Namtolea Yesu”, kwa ajili ya ibada, kuimba na kujifunza.
Maneno ya Wimbo
Yote namtolea Yesu
Nampa moyo wote,
Nitampenda siku zote,
Namwandama kila saa.
Yote kwa Yesu,
Yote kwa Yesu,
Yote kwako, Ee mwokozi,
Natoa sasa.
Yote namtolea Yesu,
Nainamia pake;
Nimeacha na anasa,
Kwako Yesu nipokee,
Yote namtolea Yesu,
Nifanye niwe wako;
Nipe Roho yako, Bwana,
Anilinde daima,
Yote namtolea Yesu,
Nami naona sasa;
Furaha ya ukombozi,
Nasifu jina lake,