Tenzi za Rohoni 20 – Ninaye Rafiki naye

Tenzi za Rohoni 20 – Ninaye Rafiki naye

Tenzi Na. 20

Soma maneno kamili ya Tenzi za Rohoni namba 20, “Ninaye Rafiki naye”, kwa ajili ya ibada, kuimba na kujifunza.


Maneno ya Wimbo

Ninaye Rafiki naye
Alinipenda mbele;
Kwa kamba za pendo zake
Nimefungwa milele;
Aukaza moyo wangu,
Uache mageule,
Mimi wake, yeye wangu;
Ndimi naye milele.

Ninaye rafiki ndiye
Aliyenifilia;
Alimwaga damu yake
Kwa watu wote pia;
Sina kitu mimi tena,
Nikiwa navyo tele;
Pia vyote ni amana
Ndimi wake milele.

Ninaye rafiki naye
Uwezo amepewa;
Atanilinda mwenyewe,
Juu tachukuliwa;
Nikitazama Mbinguni,
Hupata nguvu tele;
Sasa natumika chini,
Kisha juu milele.

Ninaye rafiki naye,
Anao moyo mwema;
Ni mwalimu, kiongozi,
Mlinzi wa daima;
Ni nani wa kunitenga
Na mapenzi ya mbele?
Kwake nimetia nanga,
Ndimi wake milele.


Tazama Tenzi za Rohoni 1–164


Omba App ya Tenzi za Rohoni kwa Android

banner
Scroll to Top