Tenzi za Rohoni 21 – Roho Yangu Hima

Tenzi za Rohoni 21 – Roho Yangu Hima

Tenzi Na. 21

Soma maneno kamili ya Tenzi za Rohoni namba 21, “Roho Yangu Hima”, kwa ajili ya ibada, kuimba na kujifunza.


Maneno ya Wimbo

Roho yangu hima, na taa yako
Kaiwashe vyema, hapa si pako;
Nguvu zote pia za duniani
Hazitakudhuru ukiamini.

Yesu yuko mbele, Yesu yu nyuma,
Yesu vivyo kando, walindwa vyema.

Adui shetani, na nguvu zake,
Bwana ameshinda, kwa kifo chake;
Wewe nguvu huna, huna kabisa,
Ndiwe mpungufu, mnyonge hasa.

Toka na mapema, mbele ya wote,
Omba, bisha sana, maisha yote;
Vita vikaliko, macho ukae,
Jivike silaha, nawe sishindwe.

Bwana Yesu ndiye kwako mchunga,
Neno lake Bwana ndilo upanga;
Mbingu zitakwisha, na nchi pia,
Neno lake Bwana laendelea.


Tazama Tenzi za Rohoni 1–164


Omba App ya Tenzi za Rohoni kwa Android

banner
Scroll to Top