Tenzi za Rohoni 11 – Nina haja nawe
Tenzi Na. 11
Soma maneno kamili ya Tenzi za Rohoni namba 11, “Nina haja nawe”, kwa ajili ya ibada, kuimba na kujifunza.
Maneno ya Wimbo
Nina haja nawe
Kila saa;
Hawezi mwingine
Kunifaa.
Yesu, nakuhitaji
Vivyo kila saa!
Niwezeshe, Mwokozi,
Nakujia.
Nina haja nawe;
Kaa nami,
Na maonjo haya,
Hayaumi.
Nina haja nawe;
Kila hali,
Maisha ni bure,
Uli mbali.
Nina haja nawe,
Nifundishe
Na ahadi zako
Zifikishe.
Nina haja nawe,
Mweza yote,
Ni wako kabisa
Siku zote.