Tenzi za Rohoni 5 – Jina lake Yesu tamu

Tenzi za Rohoni 5 – Jina lake Yesu tamu

Tenzi Na. 5

Soma maneno kamili ya Tenzi za Rohoni namba 5, “Jina lake Yesu tamu”, kwa ajili ya ibada, kuimba na kujifunza.


Maneno ya Wimbo

Jina lake Yesu tamu;
Tukilisikia
Hutupoza, tena hamu
Hutuondolea.

Roho iliyoumia
Kwalo hutibika,
Chakula, njaani pia;
Raha, tukichoka.

Jina hili ni msingi,
Ngao, ngome, mwamba,
Kwa hili napata wingi,
Kwangu ni akiba.

Yesu, Mchunga, Rafiki
Mwalimu, Kuhani,
Mwanzo, Mwisho, Njia, Haki,
Uzima kifoni.

Moyo wangu hauwezi,
Kukusifu kweli,
Ila sifa zangu hizi,
Bwana zikubali.

Na utakaponiita,
Kuja kwako Bwana,
Huko kwako sitaacha
Kukusifu sana.


Tazama Tenzi za Rohoni 1–164


Omba App ya Tenzi za Rohoni kwa Android

banner
Scroll to Top