Tenzi za Rohoni 4 – Jina La Yesu Salamu!

Tenzi za Rohoni 4 – Jina La Yesu Salamu!

Tenzi Na. 4

Soma maneno kamili ya Tenzi za Rohoni namba 4, “Jina La Yesu Salamu!”, kwa ajili ya ibada, kuimba na kujifunza.


Maneno ya Wimbo

Jina la Yesu, Salamu!
Lisujudieni,
Ninyi Mbinguni, hukumu
Na enzi mpeni.

Enzi na apewe kwetu,
Watetea dini;
Mkuzeni Bwana wenu,
Na enzi mpeni.

Enyi mbegu ya rehema,
Nanyi msifuni;
Mmeponywa kwa neema,
Na enzi mpeni.

Wenye dhambi kumbukeni
Ya msalabani,
Kwa furaha msifuni,
Na enzi mpeni.

Kila mtu duniani
Msujudieni,
Kote-kote msifuni,
Na enzi mpeni.

Sisi na wao pamoja
Tu mumo sifani,
Milele sifa ni moja,
Ni “Enzi mpeni.”


Tazama Tenzi za Rohoni 1–164


Omba App ya Tenzi za Rohoni kwa Android

banner
Scroll to Top