Tenzi za Rohoni 2 – Twamsifu Mungu
Tenzi Na. 2
Soma maneno kamili ya Tenzi za Rohoni namba 2, “Twamsifu Mungu”, kwa ajili ya ibada, kuimba na kujifunza.
Maneno ya Wimbo
Twamsifu Mungu kwa Mwana wa Pendo,
Aliyetufia na kupaa juu.
Aleluya! Usifiwe; Aleluya! Amin.
Aleluya! Usifiwe, utubariki.
Twamsifu Mungu kwa Roho Mtukufu,
Ametufunulia Mwokozi wetu.
Twamsifu Mwana, aliyetufia,
Aliyetwaa dhambi akazifuta.
Twamsifu Mungu wa neema yote,
Ametukomboa akatuongoza.
Tuamshe tena, tujazena pendo,
Na moyoni uwashe moto wa Roho.