Tenzi za Rohoni 1 – Mwokozi Umeokoa
Tenzi Na. 1
Soma maneno kamili ya Tenzi za Rohoni namba 1, “Mwokozi Umeokoa”, kwa ajili ya ibada, kuimba na kujifunza.
Maneno ya Wimbo
Mwokozi umeokoa,
Nimekuwa wako wewe.
Damu imenisafisha;
Sifa kwa mwana Kondoo.
Utukufu, Aleluya!
Sifa kwa Mwana Kondoo!
Damu imenisafisha,
Utukufu kwa Yesu!
Nilijitahidi sana
Ila sikupata raha;
Bali kwa kumtegemea
Nilipata Baraka.
Daima namwegemea
Damu ikifanya kazi,
Nikioga kwa chemichemi
Itokayo Mwokozi.
Sasa nimewekwa wakfu;
Nitaishi kwako wewe:
Fahari nashuhudia
Ya wokovu wa bure.
Nasimama kwake Yesu,
Ameponya roho yangu;
Ameniondoa dhambi,
Anifanye mzima.
Nilikuwa kifungoni,
Niliteswa na dhambi,
Nilifungwa minyororo
Yesu akanifungua.
Sifa, ameninunua!
Sifa, nguvu za wokovu!
Sifa, Bwana huhifadhi!
Sifa zake milele.