Kiswahili Form One Notes – Ufahamu

Kiswahili Form One Notes – Ufahamu

Full text version of Kiswahili Form One Notes on Ufahamu, transcribed from the supplied source document. Source images are intentionally omitted; all recognized text from the topic pages is included below.

Full text: This page contains the complete recognized text for source pages 29-32. For the original PDF layout and illustrations, use the WhatsApp button below.
—————
‘Kiswahili kidato cho kwanza

MADA YA NANE: UFAHAMU

Ufahamu ni dhana inayorejelea kujua na kulielewa jambo kwa usahihi na kuweza kulielezea
upya kwa usahihi bila kupoteza maana yake ya msingi. Ufahamu wa mtu waweza kupimwa
katika kusikiliza jambo au katika kusoma
Kusikiliza
Ufahamu wa kusikiliza ni zaidi ya kusikiliza tu kile kilichosemwa; badala yake ni uwezo wa mtu
kuelewa maana ya maneno anayoyasikia na kuweza kuhusiana nayo kwa namna fulani. Kwa
mfano mwanafunzi anaposikiliza hadithi, ufahamu mzuri Wa kusikiliza humsaidia kuiclewa
hadithi hiyo, kuikumbuka, kuijadili, na hata kuisimulia tena kwa maneno yake mwenyewe.
Mambo ya Kuzingatia katika Ufahamu wa Kusikiliza
Elezea mambo ya kuzingatia katika ufahamu wa kusikiliza
Ufahamu wa kusikiliza unahusisha michakato kadhaa katika kuelewa na kupata maana ya kile
kinachozungumzwa. Michakato hii inahusisha:
+ Kuclewa vizuri sarufi ya lugha ile inayozungumzwa
+ Kuelewa vyema maana ya maneno ya mhusiaka anayezungumza
+ Kuelewa sintaksia (muundo wa maneno) ya sentensi kwa namna zinavyowasilishwa.
Katika ufahamu wa kusikiliza, msikilizaji hana budi kuzingatia mambo yafutayo:
1. Kuwa makini na kuelekeza akili yote kwa mzungumzaji ili kuweza kusikia kila
anachokisema.
2. Kutilia maanani vidokezo vya mana ili kubaini iwapo msemaji anaongeza jambo jipya,
anatofautisha, anafafanua au anahitimisha hoja.
3. Msomaji anatakiwa kuandika baadhi ya mambo anayoona kuwa ni ya muhimu ili
kumasidia kukumbuka hapo baadae.
4, Kuwa makini na ishara mbambali_ za mwili kama vile kurusha mikono, kutingisha
kichwa, kutingisha mabega au hata kupepesa macho. Ishara hizi huwa zinachangia kwa
kiasi kikubwa kupata maana katika mazungumzo.
Kujibu Maswali kutokana na Habari uliyosikiliza
Jibu maswali kutokana na habari uliyosikiliza
Zoedi 1
Jibu maswali kutokana na habari uliyosikiliza
Kusoma kwa Sauti
Kusoma kwa sauti ni namna ya kuyaangalia maandishi na kuyatamka kwa sauti inayosikika,
Mambo ya Kuzingatia katika Ufahamu wa Kusoma
Elezea mambo ya Kuzingatia katika ufahamu wa kusoma kwa sauti
Kuna vipengele viwili vinavyounda mchakato wa ufahamu wa kusoma:
‘+ Uelewa wa msamiati na
+ Uelewa wa matini
© twshole 2019 | twhvleegmeil.com
ji_——-—_—-——-——-—-—- —_—________————————
—————
‘Kiswahili kidato cha kwanza
Ii kuilelewa habari/matini ni lazima msomaji awe na uwezo wa kuelewa msamiati uliotumika
katikamatinihiyo, Endapo maneno yaliyotumika hayataeleweka vilevile matini yote
haitaeleweka.
Katika ufahamu wa kusoma, msomaji anatakiwa kuzingatia mambo yafuatayo:
1. Kubaini mawazo makuu; msomaji anaposoma habari fulani au kitabu inatakiwa
ajiulize, Je, kinachoongelewa hapa ni nini? Ni jambo gani hasa analolizungumzia
‘mwandishi? Msomaji akiwa na maswali haya akilini mwake basi itakuwa rahisi kwake
kkuiclewa habari hiyo.
2. Kuzingatia alama za uakifishi; msomaji ni lazima azingatie alama za vakifishi, kwa
‘kufanya hivyo itamsaidia kuclewa ujumbe wa’habari hiyo navendapo hatazingatia alama
za wakifishaji anaweza kupotosha maana ya mwandishi.
3. Kubaini maana ya maneno na misemo mbalimbali; habari nyingine huwa zina
maneno ya kisanaa hivyo ni muhimu msomaji kubaini maana ya maneno hayo katika
muktadha wa habari hiyo, hii itamsaidia kuelewa vyema maana ya mwandishi,
4. Vilevile msomaji anatakiwa kumakinikia kile anachokisoma, kila kipengele
anachokisoma inampasa akielewe vizuri.
Kwa kuzingatia haya yote msomaji atakuwa na uelewa mzuri ju ya habari aliyoisoma na pia
anaweza kufupisha habari hiyo aliyoisoma
Jibu maswali kutokana na habari uliyosoma
Kusoma Kimya
Kujibu Maswali kutokana na Habari ulivoisoma
Katika usomaji huu, msomaji hufumba kinywa na kupitisha macho katika kila mstari
harakaharaka. Macho hayo huunganisha neno lililotangulia na lile linalofuata. Ubongo wake
huchambua mambo muimu yanayojitokeza, huku akiyahifadhi kichwani. Mtu akijizoeza kusoma
kimya, ananufaika ifuatavyo:
a. Hupata nafasi ya kupima mwendo wake na kiasi cha welewa
b. Hujiepusha na lawama ya kusumbua wengine
¢. Hukwepa kuzingatia kanuni za matamshi
4. Huweza kusoma maandishi mengi kuliko ambavyo angesoma kwa sauti
Kusoma kwa Burudani
Huu ni usomaji ambao’lengo lake kun huwa ni kujiburudisha tu, Katika usomaji wa aina hii,
‘msomaji hujisomea zaidi magazeti, majarida na vitabu tofauti na vile vinavyotumika darasani
Mambo ya Kuzingatiwa katika Ufahamu wa Kusoma kwa Burudani
Fafanua mambo ya kuzingatiwa katika ufahamu wa kusoma kwa burudani
Wakati mwingine sio lazima msomaji awe na vitabu vyote ambavyo anahitaji kuvisoma au
magazeti na majarida. Inapotokea hivyo, msomaji anaweza kwenda maktaba kuazima kitabu
nachokihitaji
Ingawa lengo la msomaji huwa ni kujiburudisha tu, lakini pia hujiongezea maarifa. Hii ni kwa
sababu, magazeti, majarida na vitabu sambamba na kutuamia lugha sanifu huelezea mambo
mabalimbali yanayoihusu jamii.
© twshole 2019 | twhvleegmeil.com
ji_——-—_—-——-——-—-—- —_—________————————
—————
‘Kiswahili kidato cha kwanza
Hivyo msomaji kutokana na kusoma vitabu na majarida mbalimbali hujiongezea kiwango cha
welewa wa lugha na mambo mengine ya kijamii yanayojadiliwa humo,
Ni jambo zuri kwa msomaji kujijengea tabia ya kujipima ili aweze kuelewa kiwango cha maarifa
aliyopata katika kujisomea. Kujipima huku kunaweza kufanywa kwa kujiundia utaratibu wa
kuweka kumbukumbu ya vitu au makala zilizosomwa na kufanya ufupisho wa kila makala
Utaratibu unaopendekezwa katika kujipima na kujiwekea kumbukumbu ya usomaji wa burudani
ni kama ufuatao:
1. Tarche…
2. Jina la kitabu/makala/gazeti….
3. Mchapishaji..
4. Mwaka/tarche ya uchapishaji,
5. Ufupisho wa habari( yasizidi maneno 20)
6. Fundisho/ujumbe mkuu ni…
7. Jambo lililokuvutia sana…
8. Maoni kwa ujumla kama yapo.
© twshole 2019 | twhvleegmeil.com
ji_——-—_—-——-——-—-—- —_—________————————

GET ORIGINAL PDF NOTES THROUGH 255620339260

banner
Scroll to Top