Vyuo Vinavyotoa Kozi za Diploma Zenye Mkopo wa HESLB Tanzania
Orodha rasmi ya vyuo vya serikali na binafsi vinavyotoa kozi za stashahada (diploma) zilizopewa kipaumbele cha mkopo na Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) kwa mwaka wa masomo 2026/2027.
Maswali Yanayoulizwa Mara kwa Mara (FAQs)
Wanafunzi wenye sifa za kupata mkopo lazima wawe wamepata udahili katika kozi zilizopewa kipaumbele (kama vile Afya, Kilimo, ICT, Uhandisi, au Ualimu wa Sayansi/Hisabati) katika vyuo vinavyotambuliwa na NACTVET au MoEST. Lazima uwe raia wa Tanzania, uwe na umri usiozidi miaka 35 wakati wa kuomba, na uwe umekidhi vigezo vya uhitaji (means testing) baada ya kuwasilisha maombi yako SIPAS.
Hapana. HESLB inatoa mkopo kwa kozi maalum zilizotangazwa kwenye mwongozo wa kipaumbele. Kwa mfano, kozi za Afya za Cluster 1 zenye mkopo ni pamoja na Clinical Dentistry, Diagnostic Radiography, Medical Laboratory Sciences, na Physiotherapy. Kozi ya Diploma in Nursing and Midwifery ya kawaida haina mkopo wa HESLB isipokuwa ukiwa na Higher Diploma in Mental Health Nursing au ukiwa umedahiliwa katika vyuo vya serikali vilivyopewa kipaumbele cha kipekee (kama MUHAS).
Ada ya maombi ya mkopo wa diploma HESLB ni TZS 20,000/=, ambayo hulipwa mara moja kupitia mfumo wa SIPAS kwa kutumia control number inayozalishwa wakati wa kufanya maombi.
Unaweza kupata msaada wa karibu wa udahili wa vyuo, uhakiki wa vyeti vya kuzaliwa (RITA) na ujazaji wa maombi ya mkopo HESLB kupitia wataalamu wa Devine Vision Tech. Wasiliana nao kupitia WhatsApp au Piga simu namba 0620339260.
Unahitaji Msaada wa Ujazo wa Vyuo na Maombi ya Mkopo HESLB?
Usirisk kukosa chuo au kukataliwa mkopo kwa sababu ya makosa madogo ya ujazaji wa fomu au nyaraka. Timu yetu itakusaidia hatua kwa hatua:
- Ushauri wa kozi zenye uhakika wa mkopo kulingana na ufaulu wako
- Kuchagua na kuomba vyuo vyenye nafasi bila makosa
- Ujazaji na utumaji wa maombi ya mkopo HESLB kwa 100% usahihi
- Kufuatilia na kuhakikisha udahili na majina ya mikopo yakitoka
