NAMNA YA KUPATA CHETI CHA KUZALIWA MTANDAONI TANZANIA | MWONGOZO KAMILI eRITA
Namna ya Kupata Cheti cha Kuzaliwa Mtandaoni Tanzania Kupitia eRITA | Mwongozo Kamil Namna ya Kupata Cheti cha Kuzaliwa Mtandaoni Tanzania Kupitia eRITA Mwongozo kamili hatua kwa hatua – Rahisi, haraka na bila foleni! Jifunze jinsi ya kuomba cheti cha kuzaliwa online kwa wazazi, walezi au watu wazima. Cheti cha kuzaliwa ni hati muhimu sana kwa kila Mtanzania. Inahitajika kwa ajili ya kupata NIDA, pasipoti, kujiandikisha shule, ajira rasmi na huduma nyingine za serikali. Sasa unaweza kuomba cheti cha kuzaliwa mtandaoni kupitia portal rasmi ya eRITA bila kwenda ofisini – rahisi na kwa gharama nafuu. Mfano wa cheti cha kuzaliwa kilichotolewa na RITA Cheti cha Kuzaliwa ni Nini na Inafaa Nini? Cheti cha kuzaliwa ni hati rasmi inayotolewa na RITA (Registration Insolvency and Trusteeship Agency). Inathibitisha jina lako, tarehe ya kuzaliwa, mahali ulipozaliwa na majina ya wazazi. Bila cheti hiki huwezi kupata huduma nyingi muhimu kama NIDA au pasipoti. Portal Rasmi ya eRITA Tumia link rasmi pekee ili kuepuka ulaghai: 👉 https://erita.rita.go.tz Hatua 1: Fungua Browser na Nenda Google Chukua simu au kompyuta yenye intaneti, fungua browser (Chrome au Firefox) na utafute “RITA” au moja kwa moja fungua link rasmi hapo juu. Tafuta “eRITA” au “RITA Tanzania” kwenye Google na ubonyeze link rasmi Hatua 2: Kufungua eRITA Portal Ukifika kwenye portal, utaona vitufe vya “Register an account” au “Sign in”. Ukurasa wa kwanza wa eRITA – Bonyeza Register au Sign in Hatua 3: Kujisajili au Kuingia Akaunti Kama huna akaunti: Bonyeza Register na jaza jina, email, namba ya simu na password. Thibitisha kupitia email au SMS. Kama una akaunti: Ingia kwa email na password. Fomu ya usajili au sign in kwenye eRITA Hatua 4: Nenda Birth Services na Anza Application Mpya Baada ya kuingia, bonyeza “Birth Services” kushoto, kisha “Start a New Application”. Chagua “New Birth Certificate”. Chagua Birth Services na anza maombi mapya Hatua 5: Kujaza Fomu ya Maombi Jaza taarifa za muombaji, mtoto, mahali pa kuzaliwa, wazazi na mtoa taarifa kwa usahihi mkubwa. Mfano wa fomu ya kujaza taarifa za mtoto na wazazi Hatua 6: Chagua Ofisi ya Kuchukua Cheti na Pakia Nyaraka Chagua mkoa na wilaya ya ofisi ya RITA. Pakia notification of birth, vitambulisho vya wazazi n.k. Hatua 7: Malipo na Upload Fomu Iliyosainiwa Lipa kupitia control number (mobile money au benki). Pakua fomu, saini na upakie tena. Tahadhari: Jaza taarifa kwa usahihi ili maombi yasirudishwe. Tumia link rasmi pekee! Video ya Maelekezo Kamil Tazama video hii kwa maelezo ya moja kwa moja hatua kwa hatua: Manufaa ya Kuomba Mtandaoni Huduma ni rahisi na inapatikana popote ulipo Hakuna foleni ndefu ofisini Inakuokoa muda na gharama za usafiri Ufuatiliaji wa maombi mtandaoni Anza Maombi Yako Sasa Usisubiri! Tumia portal rasmi ya eRITA ili kupata cheti cha kuzaliwa kwa urahisi. 🔗 Fungua eRITA Portal Sasa – erita.rita.go.tz Pata Notes Mpya, Maswali Zaidi, Mitihani Mingi na Huduma Nyingine Unahitaji notes mpya za masomo, maswali, au past papers? Bonyeza hapa chini na tutakuunganisha na linki yenye notes na maswali papo hapo au tupigie simu. Huduma za Kutengeneza Ripoti, Document za Utafiti (Research), Vitabu, Assessment Plan, Stationery, Utengenezaji wa Kompyuta, Mahitaji ya Software na huduma zingine nyingi. Tuma ujumbe wa WhatsApp “BURE” ili tuweze kukuhudumia mara moja! Tuma Ujumbe WhatsApp Piga Simu: 0620 339 260 © 2026 Devine Vision Tech | Huduma za Kitaalamu kwa Watanzania
