Tenzi za Rohoni 85 – Ni “Mtu Wa Simanzi”
Tenzi Na. 85
Soma maneno kamili ya Tenzi za Rohoni namba 85, “Ni “Mtu Wa Simanzi””, kwa ajili ya ibada, kuimba na kujifunza.
Maneno ya Wimbo
Ni “Mtu wa Simanzi”,
Mwana wa mwenye enzi
Mwenye mengi mapenzi!
Asifiwe Bwana Yesu!
Akawa matesoni,
“Mungu mwana yakini
Akatoka Mbinguni:
Asifiwe Bwana Yesu!
Akapata dhihaka,
Mzoea – mashaka
Ndiye yetu sadaka:
Asifiwe Bwana Yesu!
Tu wenye dhambi sana;
Kwake dhambi hamna,
Na Mungu twapatana:
Asifiwe Bwana Yesu!
Alikufa mtini,
Akalia dhikini,
Sasa yuko Mbinguni:
Asifiwe Bwana Yesu!
Punde atarejea,
Yesu kutunyakua,
Ndipo tutamwimbia:
Asifiwe Bwana Yesu!