Tenzi za Rohoni 62 – Bwana Wa Mabwana
Tenzi Na. 62
Soma maneno kamili ya Tenzi za Rohoni namba 62, “Bwana Wa Mabwana”, kwa ajili ya ibada, kuimba na kujifunza.
Maneno ya Wimbo
Bwana wa mabwana,
Mwenye nguvu sana
Twakusihi:
Neno la milele
Na liende mbele,
Waongoke tele
Kwa Mwokozi.
Tunaowaona
Wanavyopatana,
Kulipinga,
Hawataliweza
Neno, kulitweza:
Huwaje! Kucheza:
Na upanga?
Heri wajitunze
Ili wapatane,
Na Mwokozi;
Watafute sana,
Wapate kuona,
Yesu kuwa Bwana,
Mkombozi.
Mungu awaita
Wasije kukuta
Pigo lake;
Hakuona vyema
Wakose uzima,
Awape rehema,
Waokoke.
Mwenye utukufu
Tunamshukuru
Yeye pweke!
Nasifiwe sana,
Baba, naye Mwana,
Na wa tatu tena
Roho yake.