Tenzi za Rohoni 38 – Twende Kwa Yesu
Tenzi Na. 38
Soma maneno kamili ya Tenzi za Rohoni namba 38, “Twende Kwa Yesu”, kwa ajili ya ibada, kuimba na kujifunza.
Maneno ya Wimbo
Twende kwa Yesu mimi nawe,
Njia atwonya tuijue
Imo Chuoni; na Mwenyewe,
Hapa asema, Njoo!
Na furaha tutaiona,
Mioyo ikitakata sana,
Kwako, Mwokozi, kuonana,
Na milele kukaa.
“Wana na waje”, atwambia,
Furahini mkisikia,
Ndiye mfalme wetu pia,
Na tumtii, Njoo.
Wangojeani? Leo yupo;
Sikiza sana asemapo;
Huruma zake zikiwapo,
Ewe kijana, Njoo.