Tenzi za Rohoni 34 – Njoni Wenye Dhambi

Tenzi za Rohoni 34 – Njoni Wenye Dhambi

Tenzi Na. 34

Soma maneno kamili ya Tenzi za Rohoni namba 34, “Njoni Wenye Dhambi”, kwa ajili ya ibada, kuimba na kujifunza.


Maneno ya Wimbo

Njoni! Njoni! Wenye dhambi,
Njoni, msikawie;
Yesu awangojea ndiye awapendaye;
Ajuaye awezaye
kuwaponya ni Yeye.
Ewe muhitaji uje;
Anakukaribisha,
Imani, kweli, na toba,
Neema ya kutosha,
Jua sana, kwake Bwana
Bure utapata.
Njoni, mliolemewa
Na dhambi ya Adamu;
Mkingoja kujiponya
Mtapotea mumu;
Si wa haki, ni wakosa
Waoshwao kwa damu.
Ikamtokea dhiki,
Mle Gethisemani;
Kisha alipoangikwa
Akalia mtini;
” Imekwisha”, alitosha
Dhabihu ya thamani.
Kristo aliye Mbinguni
Hutuombea huko;
Basi mtumai yeye;
Kamwe mwingine hako
Yesu pweke, Yesu pweke,
Ndiye Mwokozi wako.
Wamsifu-sifu sana
Mbinguni malaika;
Wachanganya nyimbo zao
Na waliookoka:
Aleluya wataimba
Waliooshwa taka.


Tazama Tenzi za Rohoni 1–164


Omba App ya Tenzi za Rohoni kwa Android

banner
Scroll to Top