Tenzi za Rohoni 25 – Nimekombolewa na Yesu
Tenzi Na. 25
Soma maneno kamili ya Tenzi za Rohoni namba 25, “Nimekombolewa na Yesu”, kwa ajili ya ibada, kuimba na kujifunza.
Maneno ya Wimbo
Nimekombolewa na Yesu
Aliyenirehemia;
Kwa bei ya mauti yake
Nimekuwa mtoto wake.
Kombolewa!
Nakombolewa na damu;
Kombolewa!
Mimi mwana wake kweli.
Kukombolewa nafurahi,
Kupita lugha kutamka;
Kulionyesha pendo lake,
Nimekuwa mtoto wake.
Nitamwona uzuri wake,
Mfalme wangu wa ajabu;
Na sasa najifurahisha,
Katika neema yake.
Najua taji imewekwa
Mbinguni tayari kwangu;
Muda kitambo atakuja,
Ili alipo, niwepo.