Tenzi za Rohoni 10 – Usinipite!

Tenzi za Rohoni 10 – Usinipite!

Tenzi Na. 10

Soma maneno kamili ya Tenzi za Rohoni namba 10, “Usinipite!”, kwa ajili ya ibada, kuimba na kujifunza.


Maneno ya Wimbo

Usinipite Mwokozi,
Unisikie;
Unapozuru wengine,
Usinipite.

Yesu,Yesu,
Unisikie;
Unapozuru wengine,
Usinipite.

Kiti chako cha rehema,
Nakitazama;
Magoti napiga pale,
Nisamehewe.

Sina ya kutegemea,
Ila Wewe tu;
Uso wako uwe kwangu;
Nakuabudu.

U Mfariji peke yako;
Sina Mbinguni,
Wala duniani pote,
Bwana mwingine.


Tazama Tenzi za Rohoni 1–164


Omba App ya Tenzi za Rohoni kwa Android

banner
Scroll to Top