Tenzi za Rohoni 9 – Yesu kwetu ni rafiki

Tenzi za Rohoni 9 – Yesu kwetu ni rafiki

Tenzi Na. 9

Soma maneno kamili ya Tenzi za Rohoni namba 9, “Yesu kwetu ni rafiki”, kwa ajili ya ibada, kuimba na kujifunza.


Maneno ya Wimbo

Yesu kwetu ni rafiki,
Hwamiwa haja pia;
Tukiomba kwa Babaye
Maombi asikia;
Lakini twajikosesha,
Twajitweka vibaya;
Kwamba tulimwomba Mungu
Dua angesikia.

Una dhiki na maonjo?
Una mashaka pia.
Haifai kufa moyo,
Dua atasikia
Hakuna mwingine mwema
Wa kutuhurumia;
Atujua tu dhaifu;
Maombi asikia.

Je, hunayo hata nguvu,
Huwezi kuendelea,
Ujapodharauliwa
Ujaporushwa pia,
Watu wange kudharau,
Wapendao dunia,
Hukwambata mikononi,
Dua atasikia.


Tazama Tenzi za Rohoni 1–164


Omba App ya Tenzi za Rohoni kwa Android

banner
Scroll to Top