Tenzi za Rohoni 8 – Taji mvikeni

Tenzi za Rohoni 8 – Taji mvikeni

Tenzi Na. 8

Soma maneno kamili ya Tenzi za Rohoni namba 8, “Taji mvikeni”, kwa ajili ya ibada, kuimba na kujifunza.


Maneno ya Wimbo

Taji mvikeni,
Taji nyingi tena,
Kondoo mwake kitini,
Bwana wa mabwana;
Name tamsifu
Alikufa kwangu,
Ni mfalme mtukufu,
Mkuu wa Mbingu.

Taji mvikeni
Mwana wa bikira;
Anazovaa kichwani
Aliteka nyara;
Shiloh wa wanabii,
Mchunga wa watu,
Shina na tanzu vya Yese,
Wa Bethirehemu.

Taji mvikeni
Bwana wa mapenzi;
Jeraha zake ni shani
Ni vito vya enzi,
Mbinguni hakuna
Hata malaika
Awezaye kuziona
Pasipo kushangaa.


Tazama Tenzi za Rohoni 1–164


Omba App ya Tenzi za Rohoni kwa Android

banner
Scroll to Top