Tenzi za Rohoni 7 – Ni Tabibu Wa Karibu
Tenzi Na. 7
Soma maneno kamili ya Tenzi za Rohoni namba 7, “Ni Tabibu Wa Karibu”, kwa ajili ya ibada, kuimba na kujifunza.
Maneno ya Wimbo
Ni tabibu wa karibu;
Tabibu wa ajabu;
Na rehema za daima;
Ni dawa yake njema.
Imbeni, malaika,
Sifa za Yesu Bwana;
Pweke limetukuka
Jina lake Yesu.
Hatufai kuwa hai,
Wala hatutumai,
Ila kweli yeye ndiye
Atupumzishaye.
Dhambi pia na hatia
Ametuchukulia;
Twendeni na amani
Hata kwake Mbinguni.
Huliona tamu jina
La Yesu Kristo Bwana,
Yuna sifa mwenye kufa
Asishindwe na kufa.
Kila mume asimame,
Sifa zake zivume;
Wanawake na washike
Kusifu jina lake.
Na vijana wote tena,
Wapendao sana
Waje kwake wawe wake
Kwa utumishi wake.