Tenzi za Rohoni 6 – Baba, Mwana, Roho

Tenzi za Rohoni 6 – Baba, Mwana, Roho

Tenzi Na. 6

Soma maneno kamili ya Tenzi za Rohoni namba 6, “Baba, Mwana, Roho”, kwa ajili ya ibada, kuimba na kujifunza.


Maneno ya Wimbo

Baba, Mwana, Roho, Mungu mwenye enzi,
Kila tukiamka tunakuabudu
Baba, Mwana, Roho, Mungu wa mapenzi,
Ewe Utatu, tunakusifu.

Baba, Mwana, Roho, wakuaminio
Wanakutolea shukrani zao
Wanakusujudia malaika nao:
Wewe u mwanzo, nawe u mwisho.

Baba, Mwana, Roho, sisi tu gizani,
Utukufu wako hatuoni kosa;
U Mtakatifu, nawe u mapenzi,
U peke yako, mwenzio huna.

Baba, Mwana, Roho, Mungu mwenye enzi,
Ulivyoviumba vyote vyakusifu:
Baba, Mwana, Roho, Mungu wa mapenzi
Ewe Utatu, tunakusifu.


Tazama Tenzi za Rohoni 1–164


Omba App ya Tenzi za Rohoni kwa Android

banner
Scroll to Top