Ndoto Yako ya Uhandisi na Sayansi Itatimia MUST
Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya (MUST) ndicho kitovu cha teknolojia Tanzania. Kuanzia Uhandisi wa Takwimu (Data Science) hadi Teknolojia ya Viumbe (Biotechnology), hapa ndipo safari yako ya kimataifa inapoanzia.
ANGALIZO KWA WAOMBAJI 2026
Kiwango cha chini cha kujiunga (Institutional Points) ni Pointi 4.0. Kwa kozi za Uhandisi, lazima uwe na ufaulu wa D katika Basic Mathematics na Physics ngazi ya O-Level. Usipoteze muda kuomba kama hukidhi vigezo hivi!
Main Campus – Mbeya City
Kozi za ICT na Teknolojia
B.Eng in Data Science KIPEKEE
MB017Hii ni kozi adimu na ya kisasa. Inakuandaa kuwa mtaalamu wa kuchambua “Big Data” na kutengeneza mifumo ya akili mnemba (AI). Inachukua miaka 4.
Sifa: Passes in Advanced Math and Physics.
Bachelor of Computer Science
MB010Inajikita kwenye kutengeneza programu (Software Development) na mifumo ya kompyuta. Miaka 3.
Sifa: Passes in Advanced Math and Physics/Chemistry.
BSc in ICT
MB011Kozi inayochanganya usimamizi wa habari na teknolojia ya mawasiliano. Miaka 3.
B.Eng in Telecommunication Systems
MB009Inahusu mifumo ya mawasiliano ya simu, satelaiti na mitandao. Inachukua miaka 4.
Uhandisi na Ujenzi (Technical Education)
MUST ni mabingwa wa kozi za “Technical Education” zinazokupa ujuzi wa uhandisi na ufundishaji.
B.Technical Ed in Electrical & Electronics
Inaandaa mafundi sanifu wa mifumo ya umeme. Miaka 4.
B.Technical Ed in Civil Engineering
Usimamizi wa ujenzi wa barabara, madaraja na majengo. Miaka 4.
B.Technical Ed in Architectural Engineering
Sanaa na sayansi ya kusanifu majengo (Architecture). Miaka 4.
B.Technology in Landscape Architecture KIPEKEE
Usanifu wa mazingira ya nje na bustani za kisasa. Miaka 4.
Sayansi Asilia na Maabara
BSc in Biotechnology KIPEKEE
MB022Hii ni kozi ya sayansi ya viumbe hai kwa kutumia teknolojia. Inatumika kwenye tiba na kilimo cha kisasa. Miaka 3.
B.Laboratory Sciences and Technology
MB008Inaandaa wataalamu wa maabara za kisasa za viwandani na hospitali. Miaka 3.
Food Science
Natural Resources
Environmental Tech
Rukwa Campus College
Bachelor of Business Administration
Kozi pekee ya biashara inayotolewa MUST, inapatikana Kampasi ya Rukwa pekee. Miaka 3.
Bachelor of Mechanical Engineering
Inahusu mitambo na injini. Inapatikana pia Rukwa. Inachukua miaka 4.
Muhtasari wa Kapasiti (Admission Capacity)
| Kozi | Code | Duration | Nafasi (Capacity) |
|---|---|---|---|
| Agribusiness Management | MB020 | 3 Yrs | 200 |
| BSc with Education | MB007 | 3 Yrs | 160 |
| B.Lab Sciences | MB008 | 3 Yrs | 130 |
| Technical Ed (Civil) | MB014 | 4 Yrs | 120 |
| Data Science Engineering | MB017 | 4 Yrs | 50 |
Ushauri wa Kitaalamu wa Bure!
Je, unakwama kuchagua kozi inayendana na pointi zako? Au unahitaji msaada wa kutumia mfumo wa SIMS wa chuo? Usihangaike peke yako, timu yetu ya ushauri ipo hapa kukusaidia.
Mawasiliano: 0620 339 260 | Devine Vision Tech
