Mwongozo Kamili wa Kufuzu Ajira Portal kwa Watu Wote
Soma mwongozo wa kina zaidi nchini Tanzania unaoelezea hatua kwa hatua jinsi ya kujiandikisha, kuandaa nyaraka, kuandika wasifu (CV) inayoaminika, na mbinu za ushindi kwenye usaili wa serikali.
Mfumo wa ‘Recruitment Portal’ ndio njia pekee ya ushindani wa haki katika Utumishi wa Umma.
UTANGULIZI: Mabadiliko ya Soko la Ajira Tanzania
Serikali ya awamu ya tano sasa imeanza kutangaza nafasi za ajira kwenye vitengo mbalimbali baada ya kipindi kirefu cha mpito kilichosababishwa na uhakiki wa watumishi hewa na wenye vyeti vya kughushi. Ongezeko kubwa la wahitumu kuanzia ngazi ya cheti, stashahada na shahada limesababisha soko la ajira kuwa gumu sana, lakini pamoja na ugumu huo bado kuna wahitimu wengi hawajui hatua zinazopaswa kufuata wakati wa kuomba ajira kupitia mifumo ya kisasa.
Ikumbukwe kuwa kwa sasa serikali inatumia mfumo wa kielektroniki (Recruitment Portal) kutangaza nafasi za ajira na kufanyia maombi. Huu ni mfumo wa uwazi unaolenga kuhakikisha kila Mtanzania mwenye sifa anapata fursa sawa ya kutumikia nchi yake bila upendeleo. Hata hivyo, kutokujua mbinu za kiufundi za mfumo huu kumepelekea wahitimu wengi wenye sifa nzuri kuachwa (short-listed) kwa makosa madogo ya kiufundi.
MAMBO 10 YA KUZINGATIA WAKATI WA KUFANYA MAOMBI MTANDAONI
Haya ni maelekezo ya kina juu ya hatua zinazopaswa kufuatwa wakati wa kuomba nafasi za ajira kupitia ‘recruitment portal’ ili kupunguza changamoto na makosa:
Vyeti Vinavyohitajika (Original Only)
Muombaji anapaswa kuwa na vyeti halisi vinavyohitajika wakati wa kufanya maombi. ANGALIZO MUHIMU: Mfumo huu haukubali ‘result slip’, ‘transcript’ (kama mbadala wa cheti) wala ‘affidavit’ (kiapo cha kupoteza cheti) isipokuwa katika mazingira maalum yaliyoelezwa na PSRS. Lazima uwe na cheti halisi (Academic Certificate).
Baruapepe (Email) ya Kudumu
Kama muombaji hana baruapepe ‘email’, unapaswa kufungua baruapepe yako mwenyewe. Ni makosa makubwa kutumia email ya rafiki au ya ofisi ya internet (stationary). Uhifadhi neno lake la siri (password) sehemu salama kwani mchakato mzima wa kuitwa kwenye usaili utapita huko.
Kuandaa Nakala (Copies) za Vyeti
Mwombaji anapaswa kutoa copy vyeti vyote anavyohitaji kuvitumia wakati wa kufanya maombi. Mfano: Cheti cha Shahada (Degree), Advanced Diploma, Diploma, Cheti cha Ufundi (VETA), Academic Certificate ya Kidato cha Nne na cha Sita, na Cheti cha Kuzaliwa.
Picha Rasmi (Passport Size)
Muombaji apige picha (passport size) yenye mwonekano rasmi na rangi ya nyuma (background) inayoeleweka. Kisha chukua ‘soft copy’ yake na kuihifadhi kwenye vifaa maalum vya kutunza kumbukumbu kama vile Flash, Simu, au Laptop kwa ajili ya kuipakia kwenye mfumo.
Uhakiki na Muhuri wa Mwanasheria
Muombaji atatakiwa kuchukua vyeti vyako pamoja na nakala zake (copy) kisha apeleka kwa wakili au mahakamani kwa ajili ya kuhakikiwa na kugongwa muhuri wa kuthibitisha uhalali wa vyeti vyake (Certified True Copy). Hii ni hatua ya kisheria kuthibitisha kuwa nakala unayotuma ni sawa na cheti halisi.
Kuscan na Kuipa Majina Faili (PDF)
Mwombaji achukue nakala zake za vyeti zilizogongwa muhuri na aviscani ili apate ‘PDF’. Hakikisha kila cheti kinakaa kwenye kumbukumbu yake na kukipa jina linalotofautisha cheti kimoja na kingine. Mfano: Cheti cha kidato cha nne utakipa jina “Form Four.pdf”, kidato cha sita “Form Six.pdf” na Degree utakipa “Degree Certificate.pdf”.
Hifadhi ya Kielektroniki
Muombaji achukue ‘soft copy’ ya vyeti alivyo’scan’ pamoja na ‘soft copy’ ya picha ndogo ‘passport size’ kisha ahifadhi kwenye faili moja (folder) ili kurahisisha upatikanaji wa taarifa wakati wa mchakato wa ku’upload’. Hii inaepusha kuchanganya vyeti wakati wa kuomba kazi.
Usajili kwenye Tovuti Rasmi
Muombaji aingie kwenye tovuti ya Utumishi www.ajira.go.tz kisha aende sehemu ya ‘recruitment portal’ (portal.ajira.go.tz). Ingia kwa kutumia baruapepe na kisha jisajili kama mwanachama mpya. Anza kuingiza taarifa zako binafsi, taaluma, na uzoefu wa kazi kama zinavyojionesha.
Kukamilisha ‘Profile’ yako (90%+)
Muombaji afahamu kuwa kila sehemu inayohitaji cheti hususani sehemu ya taaluma ahakikishe ame’upload’ cheti chake husika. Ukimaliza hatua hizo, ukurasa (profile) yako itaonesha siyo chini ya **90%**. Ikiwa chini ya hapo, huenda kuna taarifa muhimu au vyeti hujaviweka vizuri.
Barua ya Maombi ya Kazi
Namna ya kuomba, muombaji aandike barua ya maombi ya ajira inayolenga nafasi husika (kila kazi inapaswa kuwa na barua yake). Kisha i-upload kwenye tangazo husika. Hapo utakuwa tayari umemaliza, tayari kwa kuhudhuria usaili endapo utatimizwa vigezo vya kuitwa.
MAANDALIZI YA WASIFU BINAFSI (CV) INAYOAMINIKA
Wasifu binafsi (CV) ndio kioo cha taaluma yako. Sekretarieti ya Ajira inashauri mambo yafuatayo ya kuzingatia wakati wa kuandaa CV:
Mambo ya Kuzingatia Kwenye CV:
- 1. Juu Kabisa: Mhusika ataje majina yote rasmi anayotumia kwa herufi kubwa kama yalivyo kwenye vyeti au viapo kama vipo. Epuka majina ya utani (nicknames).
- 2. Maelezo kwa Kifupi (Executive Summary): Taja matarajio yako na nini ofisi unayoombea kazi itegemee toka kwako kulingana na ujuzi wako.
- 3. Historia Binafsi: Taja Miaka yako, Jinsia, Hali ya ndoa, na Uraia wako.
- 4. Historia ya Elimu: Aeleze elimu kuanzia kiwango kikubwa cha elimu alichonacho hadi cha mwisho cha chini alichoanzia. Taja Vyuo ulivyosoma, mwaka aliohitimu na vyeti alivyotunukiwa.
Mfano: Bachelor Degree in Law (LLB) – UDSM 2012. - 5. Historia ya Uzoefu wa Kazi: Uchambuzi uanzie nafasi aliyonayo na kazi ya sasa hadi aliyoanzia kushika ikionyesha Mwajiri, Kipindi/Muda na Majukumu.
- 6. Wadhamini (Referees): Majina ya wadhamini wasiopungua watatu wenye anuani kamili za barua, email, na simu za mikononi. Inashauriwa wawe watu wa karibu kitaalamu (kama walimu wako au waajiri wa zamani).
- 7. Kiapo/Tamko na Saini: Thibitisha taarifa ulizotoa ni sahihi na za kweli. Weka saini na tarehe.
NYARAKA MUHIMU UNAPOKUJA KWENYE USAILI
Usisahau Nyaraka Hizi Siku ya Interview:
- Cheti halisi cha kuzaliwa: Kuthibitisha uraia na umri.
- Vitambulisho: NIDA, Kitambulisho cha Mkazi, Pasipoti, au Kadi ya Mpiga Kura.
- Vyeti halisi vya kitaaluma: Kuanzia Kidato cha Nne na kuendelea.
- Hati ya Kiapo: Ikiwa majina yanatofautiana kwenye nyaraka zako.
- Waliosoma Nje: Vyeti vihakikiwe na TCU, NACTE au NECTA.
ONYO:
Ni marufuku kuwasilisha taarifa za kugushi. Itakapobainika mhusika atachukuliwa hatua za kisheria mara moja.
MASHARTI YA JUMLA NA WAJIBU WA MUOMBAJI (PSRS)
| Kipengele | Maelezo na Masharti |
|---|---|
| Uraia na Kuzaliwa | Mwombaji lazima awe ni Raia wa Tanzania na aambatishe cheti cha kuzaliwa. |
| Vyeti vya Taaluma | Shahada ya juu/Shahada/Stashahada/Astashahada. Cheti cha kidato cha IV na VI ni lazima. |
| Nyaraka zisizokubalika | “Transcripts”, “Testmonials”, “Provisional Results” au FORM IV/VI RESULT SLIPS hazikubaliki kama mbadala wa cheti. |
| Umri wa Kuajiriwa | Kisheria ni miaka 45 kwa masharti ya kudumu. Zaidi ya hapo ni kwa mkataba maalum. |
| Njia ya Maombi | Uwasilishaji wa barua kwa mkono hauruhusiwi. Tumia njia ya mtandao tu kupitia Recruitment Portal. |
MASWALI YANAYOULIZWA SANA (FAQ)
Kamilisha Maombi Yako Kwa Usahihi Leo!
Kufuzu Ajira Portal ni hatua ya kwanza kuelekea ndoto yako ya Utumishi wa Umma. Ikiwa unahitaji kusaidiwa kuandaa **CV ya kitaalamu** inayokidhi viwango vya PSRS, au kuandika barua za maombi kwa ufasaha, bonyeza kitufe hapa chini.
