Ordinary Diploma in Clinical Medicine
(Stashahada ya Utabibu)
Jifunze kugundua magonjwa, kutoa tiba, na kuokoa maisha. Kuwa Tabibu (Clinical Officer) anayeaminika katika jamii.
Clinical Medicine (Utabibu) ni kozi inayoandaa wataalam wa afya wanaojulikana kama Clinical Officers (COs). Hawa ndio madaktari wa ngazi ya kati ambao hufanya kazi kubwa katika Zahanati, Vituo vya Afya, na Hospitali za Wilaya. Wana uwezo wa kutibu magonjwa mengi na kufanya upasuaji mdogo.
1. Sifa za Kujiunga (Admission Requirements)
Ili kujiunga na kozi hii kwa mwaka wa masomo 2025/2026, mwombaji lazima akidhi vigezo vya NACTVET:
- Awe na Cheti cha Kidato cha Nne (CSEE).
- Awe na ufaulu wa Alama “D” Nne (4) au zaidi.
- MASOMO YA LAZIMA: Lazima uwe na ufaulu wa alama “D” au zaidi katika masomo ya Sayansi:
- Physics (au Engineering Sciences)
- Chemistry
- Biology
- Ufaulu katika masomo ya Basic Mathematics na English Language ni sifa ya ziada.
- Japokuwa si lazima kwa vyuo vyote, kuwa na “D” ya Kiingereza na Hesabu kunakuongezea nafasi ya kuchaguliwa katika vyuo vya Serikali vyenye ushindani mkubwa.
2. Utajifunza Nini? (Core Modules)
Katika kipindi cha miaka mitatu (3), utajifunza mambo yafuatayo kwa kina:
3. Fursa za Ajira na Kujiendeleza
Clinical Officer ana wigo mpana wa kazi na kujiendeleza:
Tabibu (Clinical Officer)
Kuajiriwa katika Hospitali za Serikali, Binafsi, na Mashirika ya Dini (FBOs) kama daktari wa zamu.
AMO (Assistant Medical Officer)
Baada ya uzoefu wa kazi, unaweza kusoma kozi ya juu ya miaka 2 na kuwa AMO (Daktari Msaidizi) anayefanya upasuaji mkubwa.
Shahada ya Udaktari (MD)
Ukifaulu vizuri Diploma yako (GPA nzuri), unaweza kujiunga na Chuo Kikuu kusomea Udaktari wa Binadamu (Doctor of Medicine) kwa miaka 5.
Msimamizi wa Miradi ya Afya
Kufanya kazi na NGOs katika miradi ya kutokomeza UKIMWI, Kifua Kikuu, na Malaria vijijini.
Unahitaji Msaada wa Kujiunga?
Je, unatafuta chuo bora cha Utabibu (kama Machame, KCMC, Mvumi, Sengerema, n.k.)? Au unahitaji msaada wa kufanya maombi (Online Application)?
Sisi DeVine Vision Tech tunakusaidia kuchagua vyuo sahihi na kufanya maombi kwa umakini mkubwa ili usikose nafasi.
Fika ofisini kwetu: Kisesa, Mwanza.
