Jinsi ya Kupata Nakala ya Kitambulisho cha NIDA Online – Devine Vision Tech

Mwongozo wa Mfumo wa NIDA Mtandaoni | Devine Vision Tech
Mwongozo Kamili

Jinsi ya Kupata Nakala ya Kitambulisho cha NIDA Mtandaoni

Fahamu mchakato wa hatua kwa hatua jinsi ya kufanya usajili na kudownload nakala ya Kitambulisho chako cha NIDA kwa njia ya mtandao.

Mfano wa Kitambulisho cha Taifa NIDA Tanzania

Kitambulisho cha Taifa (NIDA) ni nyaraka muhimu sana kwa kila Mtanzania. Kinatumika kama uthibitisho wa utambulisho kwa kuwa na taarifa za kibinafsi, ikiwemo jina, tarehe ya kuzaliwa, na picha.

Kwa watu ambao bado hawajapata vitambulisho rasmi vya plastiki kutoka NIDA, wanaweza kupata nakala (copy) ya kitambulisho hiki mtandaoni. Kitambulisho hiki kina umuhimu mkubwa kwani kinasaidia katika kupata huduma za umma, huduma za kibenki, na masuala mbalimbali ya kibiashara.

Watu wengi wanatafuta kitambulisho cha NIDA kwa sababu kimekuwa kipimo cha msingi katika mitindo ya utambulisho wa raia Tanzania. Kuwa na nakala hii inasaidia pia kuondoa uwezekano wa udanganyifu au matumizi mabaya ya taarifa za watu.

Kuhifadhi Taarifa (Usalama)

Kuwepo na nakala ya mtandaoni itakuwezesha kupata taarifa zako wakati wowote na ni muhimu kuhakikisha hutapoteza kitambulisho chako cha awali.

Urahisi wa Huduma za Serikali

Kitambulisho hiki kinahitajika katika huduma nyingi za kiserikali na kibenki; hivyo nakala itarahisisha mchakato wa kupata huduma hizo haraka.

1. Mahitaji Muhimu Kabla ya Kujiandikisha

Kabla ya kuanza mchakato wa kujiandikisha mtandaoni kupitia Mfumo wa NIDA, ni muhimu kuandaa vielelezo vifuatavyo:

  • Nakala ya cheti cha kuzaliwa cha mwombaji au kiapo cha mzazi mmoja.
  • Kama uraia ni wa kurithi: Thibitisha kwa nakala ya cheti cha kuzaliwa au nakala ya kitambulisho cha Taifa cha mzazi mmoja.
  • Kama uraia ni wa kujiandikisha: Thibitisha kwa nakala ya uraia wa kujiandikisha (Dossier Number) ya mwombaji.

2. Mambo Muhimu Wakati wa Ujazaji Fomu

  • Kuwa na anuani ya barua pepe (Email) na Namba ya simu ya mkononi itakayotumika kupokea viunga vya kukamilisha usajili.
  • Kuwa na nyaraka zisizopungua mbili kuthibitisha utambulisho (Mfano: Cheti cha kuzaliwa n.k).
  • Fanya “scanning” ya nyaraka zako na kuziweka katika muundo wa PDF (usiozidi kurasa moja) au picha muundo wa JPG au PNG.
  • Kama umezaliwa Mwaka 1980 na kuendelea: Ambatisha cheti cha kuzaliwa. Kabla ya 1980: Ambatisha cheti cha kuzaliwa au “Affidavit” (Kiapo).
  • Kama una majina mengine, yaandike ili kurahisisha utambulisho iwapo kutahitajika marekebisho.
  • Fahamu majina kamili ya Baba na Mama mzazi. Ikiwa wana Namba za NIDA (NIN), weka viambata halisi vyao.
  • Jua namba ya Nyumba, Mtaa na Kata anayoishi. Kwa Watanzania walioko nje ya Nchi (Diaspora), wanatakiwa kupata uthibitisho wa ukaazi kutoka Ubalozi wa Tanzania.
  • Ambatisha vyeti vya Shule, Namba ya mlipa kodi (TIN) na Kadi ya mpiga kura (kama unavyo).

Mwombaji anatakiwa kujaza fomu kwa usahihi bila kukinzana na taarifa nyingine (kama shule au biashara). Kisha:

  1. Chapisha (Print) fomu uliyojaza mtandaoni.
  2. Nenda ofisi ya Serikali ya Mtaa kwa ajili ya kugongewa Mhuri na Saini ya Mwenyekiti wa Mtaa.
  3. Fika katika Ofisi ya NIDA ya Wilaya ukiwa na fomu iliyokamilika na nakala ngumu (hardcopies) za viambatisho vyako vyote kwa ajili ya kuchukuliwa alama za kibaiolojia.

3. Hatua za Usajili Mpya na Kupata Nakala Mtandaoni

Sehemu A: Mchakato wa Usajili Mpya (Kama Hujawahi Kusajiliwa)
1
Tembelea Tovuti na Fungua Akaunti

Tembelea NIDA Portal. Bofya “Create Account” na jaza maelezo muhimu. Thibitisha barua pepe (Email) kupitia maagizo utakayotumiwa.

2
Jaza Fomu & Tuma Viambatisho (Online)

Jaza fomu ya maombi kwa umakini. Ambatisha nyaraka za Lazima (Cheti cha kuzaliwa, Barua ya Serikali ya Mtaa, Cheti/ID ya mzazi) na za Ziada (Vyeti vya masomo, Pasi ya kusafiria, Leseni, TIN, Bima ya Afya, Kitambulisho cha Mzanzibar Mkaazi). Kisha tuma maombi.

3
Hatua za Ofisi ya NIDA Wilaya

Baada ya kujaza na ku-print mtandaoni, peleka fomu ofisi ya Wilaya. Huko utafanyiwa uhakiki, uingizaji taarifa kwenye kompyuta, na kuchukuliwa alama za vidole, picha na saini ya kielektroniki. Subiri uhakiki wa mwisho na utengenezaji wa kitambulisho.

Muonekano wa tovuti ya NIDA wakati wa kujisajili
Sehemu B: Jinsi ya Kupakua Nakala (Kama Tayari Umesajiliwa)

Baada ya maombi yako kupitishwa, unaweza kupakua nakala ya kitambulisho chako kupitia mfumo wa E-NIDA ufuatao:

1
Ingia Kwenye Akaunti Yako

Fungua tovuti ya E-NIDA Login. Bofya linki ya kuingia (Login), ingiza taarifa zako na bofya ingia.

2
Nenda Sehemu ya Kitambulisho Changu

Baada ya kuingia kwenye akaunti yako, nenda moja kwa moja kwenye menyu imeandikwa “Kitambulisho Changu” au “Identity Card Online Copy”.

3
Pakua Nakala (Download)

Katika hatua hii, kitambulisho chako kitaonekana. Bonyeza “Pakua Nakala” (au Print / Download PDF) ili kuhifadhi kitambulisho chako.

Changamoto Zinaweza Kutokea

Namba ya OTP Haifiki?

Hali hii hutokea ikiwa namba ya simu uliyoweka ni tofauti na ile iliyopo kwenye usajili. Fika ofisi za NIDA zilizo karibu nawe kwa ajili ya uhuishaji wa taarifa.

Taarifa Hazionekani?

Huenda mchakato wa usajili wako haujakamilika kikamilifu kwenye kanzidata. Unashauriwa kufuatilia kwenye ofisi za wilaya za NIDA.

Je, Unahitaji Ufafanuzi Zaidi?

Ikiwa umekumbana na changamoto yoyote katika kufuata mwongozo huu, tupo tayari kutoa ufafanuzi na ushauri wa kiufundi.

Tovuti kwa ajili ya miongozo na huduma za kiufundi.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Scroll to Top