NAMNA YA KUPATA CHETI CHA KUZALIWA MTANDAONI TANZANIA | MWONGOZO KAMILI eRITA

Namna ya Kupata Cheti cha Kuzaliwa Mtandaoni Tanzania Kupitia eRITA | Mwongozo Kamil

Namna ya Kupata Cheti cha Kuzaliwa Mtandaoni Tanzania Kupitia eRITA

Mwongozo kamili hatua kwa hatua – Rahisi, haraka na bila foleni! Jifunze jinsi ya kuomba cheti cha kuzaliwa online kwa wazazi, walezi au watu wazima.

Cheti cha kuzaliwa ni hati muhimu sana kwa kila Mtanzania. Inahitajika kwa ajili ya kupata NIDA, pasipoti, kujiandikisha shule, ajira rasmi na huduma nyingine za serikali. Sasa unaweza kuomba cheti cha kuzaliwa mtandaoni kupitia portal rasmi ya eRITA bila kwenda ofisini – rahisi na kwa gharama nafuu.

Mfano wa Cheti cha Kuzaliwa Tanzania
Mfano wa cheti cha kuzaliwa kilichotolewa na RITA

Cheti cha Kuzaliwa ni Nini na Inafaa Nini?

Cheti cha kuzaliwa ni hati rasmi inayotolewa na RITA (Registration Insolvency and Trusteeship Agency). Inathibitisha jina lako, tarehe ya kuzaliwa, mahali ulipozaliwa na majina ya wazazi.

Bila cheti hiki huwezi kupata huduma nyingi muhimu kama NIDA au pasipoti.

Portal Rasmi ya eRITA

Tumia link rasmi pekee ili kuepuka ulaghai:

Hatua 1: Fungua Browser na Nenda Google

Chukua simu au kompyuta yenye intaneti, fungua browser (Chrome au Firefox) na utafute “RITA” au moja kwa moja fungua link rasmi hapo juu.

Hatua ya kutafuta eRITA kwenye Google
Tafuta “eRITA” au “RITA Tanzania” kwenye Google na ubonyeze link rasmi

Hatua 2: Kufungua eRITA Portal

Ukifika kwenye portal, utaona vitufe vya “Register an account” au “Sign in”.

Ukurasa wa eRITA Portal
Ukurasa wa kwanza wa eRITA – Bonyeza Register au Sign in

Hatua 3: Kujisajili au Kuingia Akaunti

Kama huna akaunti: Bonyeza Register na jaza jina, email, namba ya simu na password. Thibitisha kupitia email au SMS.
Kama una akaunti: Ingia kwa email na password.

Hatua ya kujisajili eRITA
Fomu ya usajili au sign in kwenye eRITA

Hatua 4: Nenda Birth Services na Anza Application Mpya

Baada ya kuingia, bonyeza “Birth Services” kushoto, kisha “Start a New Application”. Chagua “New Birth Certificate”.

Dashboard ya Birth Services eRITA
Chagua Birth Services na anza maombi mapya

Hatua 5: Kujaza Fomu ya Maombi

Jaza taarifa za muombaji, mtoto, mahali pa kuzaliwa, wazazi na mtoa taarifa kwa usahihi mkubwa.

Kujaza fomu ya application eRITA
Mfano wa fomu ya kujaza taarifa za mtoto na wazazi

Hatua 6: Chagua Ofisi ya Kuchukua Cheti na Pakia Nyaraka

Chagua mkoa na wilaya ya ofisi ya RITA. Pakia notification of birth, vitambulisho vya wazazi n.k.

Hatua 7: Malipo na Upload Fomu Iliyosainiwa

Lipa kupitia control number (mobile money au benki). Pakua fomu, saini na upakie tena.

Tahadhari: Jaza taarifa kwa usahihi ili maombi yasirudishwe. Tumia link rasmi pekee!

Video ya Maelekezo Kamil

Tazama video hii kwa maelezo ya moja kwa moja hatua kwa hatua:

Manufaa ya Kuomba Mtandaoni

  • Huduma ni rahisi na inapatikana popote ulipo
  • Hakuna foleni ndefu ofisini
  • Inakuokoa muda na gharama za usafiri
  • Ufuatiliaji wa maombi mtandaoni

Anza Maombi Yako Sasa

Usisubiri! Tumia portal rasmi ya eRITA ili kupata cheti cha kuzaliwa kwa urahisi.

🔗 Fungua eRITA Portal Sasa – erita.rita.go.tz

Pata Notes Mpya, Maswali Zaidi, Mitihani Mingi na Huduma Nyingine

Unahitaji notes mpya za masomo, maswali, au past papers? Bonyeza hapa chini na tutakuunganisha na linki yenye notes na maswali papo hapo au tupigie simu.

Huduma za Kutengeneza Ripoti, Document za Utafiti (Research), Vitabu, Assessment Plan, Stationery, Utengenezaji wa Kompyuta, Mahitaji ya Software na huduma zingine nyingi.

Tuma ujumbe wa WhatsApp “BURE” ili tuweze kukuhudumia mara moja!

© 2026 Devine Vision Tech | Huduma za Kitaalamu kwa Watanzania

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Scroll to Top