Jinsi ya Kupata TIN Number Bure Mtandaoni Tanzania 2025
Mwongozo kamili wa hatua kwa hatua kupitia Taxpayer Portal ya TRA
TIN (Taxpayer Identification Number) ni namba ya utambulisho wa mlipakodi inayotolewa na TRA. Kupitia mwongozo huu utajifunza jinsi ya kuipata bure kabisa mtandaoni.
TIN Number ni Nini?
TIN hutumika kutambulisha mlipakodi katika mifumo ya serikali kama TAUSI, BRELA, manunuzi ya ardhi, ajira na huduma za kifedha.

Faida za Kuwa na TIN Number
- Kutambulika kisheria kama mlipakodi
- Kupata huduma za serikali kwa urahisi
- Kuepuka adhabu za kodi
- Kufanya biashara rasmi
Hatua za Kupata TIN Number Bure Mtandaoni
Hatua ya 1: Tembelea Tovuti ya TRA

Hatua ya 2: Hakiki Kama Una TIN
- Bofya Sign Up
- Chagua Check Registration Status
- Ingiza NIN yako
Hatua ya 3: Jisajili Kupitia NIN
Ingiza NIN na namba ya simu, pokea OTP, weka password na ukamilishe usajili.
Hatua ya 4: Pakua Cheti cha TIN
Nenda My Account → TIN Management kupakua TIN Certificate.
Video ya Kujifunza (Practical)
Pakua Mwongozo Rasmi wa TRA (PDF)
Mwongozo rasmi wenye picha na maelezo ya kina
Pakua PDF ya TRAMaswali Yanayoulizwa Mara kwa Mara
Je, TIN ni bure?
Ndio, TIN ni bure kabisa mtandaoni.
Ninaweza kupata bila NIN?
Kwa sasa, NIN inapendekezwa sana.
